Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
NAHODHA na mabaharia sita wa kichina ambao ni Lin Xinyong, Zoa Yongzian, Tan Yian, Xie Wenbin, Xu Kun na Mu Yong wamekutwa na hatia ya kujaribu kuua watanzania wawili mwezi uliopita kwa kuwatupa baharini kwa kile kilichoelezwa kuwa wangeweza kuwaambukiza Virusi vya Corona (Covid -19.)
Aidha mahakama hiyo imemuhukumu nahodha wa meli hiyo iliyokuwa inatoka Durban nchini Afrika Kusini Captain.Rongli kulipa faini ya Euro 4350 na kila baharia ametozwa Euro 2173.
Aidha Rongli ametozwa faini ya Euro 2175 kwa usimamizi mbovu na Euro 435 kwa kutoripoti uzamiaji uliofanywa na vijana hao na kuelekezwa kwenda jela miaka minne asipolipa faini.
Amiri Salamu (20) na Hassani Rajabu (30) walitoswa baharini baada ya kupewa life jacket na chupa mbili za maji pekee na baada ya siku mbili walijikuta katika fukwe wa utalii wa Dusk, kwa Zulu Natal kilomita 50 kutoka Kaskazini mwa Durban. Ambapo walioelekwa hospitali ambapo waaligundulika kuugua njaa, kiu na kuishiwa nguvu.
Imeelezwa kuwa mabaharia walikiri mashtaka hayo huku nahodha wa meli hiyo Rongli akikiri makosa hayo ya usafirishaji yanayohusiana na kuhatarisha maisha ya watu.
Aidha msemaji wa Mamlaka ya mashtaka ya kitaifa (NPA) Natasha Kara amesema kuwa chombo hicho kiliondoka Durban Machi 26 na siku iliyofuata kuligundulika kuwa na wanaume wawili wa kitanzania ambao ni wazamiaji ambao waliombwa wajitambulishe na kueleza kuwa walikataa kuvaa barakoa.
Aidha amesema kuwa kabla ya kutoswa baharini walipatiwa maji na vyakula na kutengwa kwenye chumba tofauti kwa kuwa hali yao ya Covid -19 haikufahamika.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo Kaimu hakimu wa mahakama Vishalan Moodley alieleza kuwa tuhuna hizo ni za majaribio ya mauaji na utekelezaji mbaya wa majukumu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment