Na Karama Kenyunko, Michuzi TV.
MFANYABIASHARA Obadia Kwitega, amehukumiwa kulipa faini ya shilingi Milioni tano ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya kukiri kosa la kuchapisha maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.
Hukumu hiyo imesomwa leo Juni 3, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Janet Mtega wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya mshtakiwa kuingia makubaliano na DPP na kukiri kosa lake hilo ambapo ametakiwa pia kulipa fidia ya sh. Milioni mbili.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mtega amesema, mahakama imetia hatiani mshtakiwa baada ya yeye mwenyewe bila kulazimishwa kuingia makubaliano na DPP ya kukiri kosa ili aweze kuwa huru.
Hata hivyo kabla ya kusomewa adhabu hiyo, mshtakiwa aliiomba mahakama isimpe adhabu kali kwa kuwa ana familia inamtegema na pia anamchumba ambaye wanatarajia kumuoa hivi karibuni.
Wakili wa serikalii, Faraji Nguka aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wanaofikiria kutenda kosa kama hilo.
Awali ilidaiwa kuwa, kati ya Januari 29 2017 na Machi 29 2019, katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam kupitia televisheni ya mtandaoni ijulikanayo kama Bongo Times TV, alichapisha maudhui bila ya kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. (TCRA) huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Mshtakiwa amefanikiwa kulipa faini hiyo na ameachiwa huru.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment