Na Woinde Shizza, KARATU
TAASISI ya Community aid and social education empowerment (CSEE) kwa kushirikiana na Child fund Korea ambao wamejikita katika kusaidia watoto dhidi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona wametoa msaada wa vifaa venye thamani ya million 40 kwa wilaya ya Karatu.
Msaada huo ni vifaa vya kukabiliana na virusi vya corona ambavyo ni pamoja na spika za sauti za kusaidia kuelimishia jamii sehemu mbalimbali zenye shughuli zinazokusanya watu wengi kwa pamoja.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo ameshukuru taasisi ya CSEE kwa msaada waliotowa kwa wananchi wa Karatu na kubainisha kuwa taasisi hiyo imegusa vijana wetu wengi hasa kwa kipindi hiki ambacho vyuo na shule za sekondari za kidato cha tano na sita zikiwa zimefunguliwa.
Alisema msaada umekuja wakati sahihi na kamati ya wilaya ya covid-19 itakaa kikao ili kuweka mpangilio mzuri wa ugawaji wa vifaa kwa watoto ma shule.
Mahongo alibainisha kuwa bado anaendelea kutoa elimu kwa watu mbalimbali juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona nakuiomba taasisi hiyo kujikita katika kambi za wavuvi tarafa ya Eyasi pamoja na sehemu za minada na kutoka elimu katika maeneo hayo
"muda mzuri wa kutoa elimu kwenye kambi ni jioni saa kumi ambao ni muda watu wengi wanakuwa wanarudi kwenye mialo pia nipongeza juhudi zilizochukuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kukabiliana na covid-19"alisema Mahongo
Afisa wa mradi wa CSEE Ombeni Sakafu alisema taasisi Yao inafanya kazi na watoto na ndio maana wakatoa vifaa ivyo kwa ajili ya kuwalinda ambapo alisema wanategemea vifaa hivyo vitasambazwa katika shule.
Alitaja vifaa walivyotoa ni pamoja na barokoa 500 N95 ,Gun themometre nne za kupima joto ,wamekabidhi box 20 za sabuni za maji ya kunawia mikono, middle’s Paddle hand wash-facilities 35 , Matanki ya kuhifadhia maji kwenye vifaa vya kunawia mikono 20, Chlorine powder kilo 126, Chlorine tablets kilo 5 za Kuna vitakasa mikono mabox 24, PPE 63, gloves boxes 83, spika 3 kwa ajili ya matangazo ya kuelimisha juu ya corona, vipeperushi 144, vienye ujumbe wa kuelimisha juu ya corona pamoja na bronchure 200 na bango 1na Face shield 333.
Aidha alisema mbali na vifaa hivyo wamejikita katika kutoa elimu kwa njia ya bodaboda ambazo watatumia vipaza sauti kucheza sauti iliyorekodiwa na wataalamu wa afya juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona.
Sakafu alibainisha kuwa watutumia wataalamu wa Halmashauri kutoa elimu ya corona kwa wananchi na watapita kwenye vijiji na magari, kutembelea kaya kuelimisha watu juu ya namna ya kujikinga na corona.
Mkuu wa wilaya ya Karatu (kushoto), Theresia Mahongo na Katibu tawala wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda wakikagua vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona juzi vilivyotolewa na Taasisi ya Community aid and social education empowerment (CSEE) ikiwemo spika kwa ajili ya kusaidia kuelisha wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha
(picha na Woinde Shizza).
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment