Na Woinde Shizza, KARATU
TAASISI ya Community Aid and Social Education Empowerment (CSEE) kwa kushirikiana na Child Fund Korea ambao wamejikita katika kusaidia watoto dhidi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona wametoa msaada wa vifaa venye thamani ya shilingi million 40 kwa Wilaya ya Karatu.
Msaada huo ni vifaa vya kukabiliana na virusi vya corona ambavyo ni pamoja na spika za sauti za kusaidia kuelimishia jamii sehemu mbalimbali zenye shughuli zinazokusanya watu wengi kwa pamoja.
Akizungumza leo Juni 4,2020, Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo ameshukuru taasisi ya CSEE kwa msaada waliotowa kwa wananchi wa Karatu na kubainisha kuwa taasisi hiyo imegusa vijana wengi hasa kwa kipindi hiki ambacho vyuo na shule za sekondari za kidato cha tano na sita zikiwa zimefunguliwa.
Amesisitiza msaada umekuja wakati sahihi na kamati ya wilaya ya Covid-19 itakaa kikao ili kuweka mpangilio mzuri wa ugawaji wa vifaa kwa watoto ma shule.
Mahongo amebainisha bado anaendelea kutoa elimu kwa watu mbalimbali juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona nakuiomba taasisi hiyo kujikita katika kambi za wavuvi tarafa ya Eyasi pamoja na sehemu za minada na kutoka elimu katika maeneo hayo
"Muda mzuri wa kutoa elimu kwenye kambi ni saa 10 jioni ambao ni muda watu wengi wanakuwa wanarudi kwenye mialo pia nipongeza juhudi zilizochukuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kukabiliana na covid-19,"amesema Mahongo
Kwa upande wake Ofisa wa Mradi wa CSEE Ombeni Sakafu amesema taasisi yao inafanya kazi na watoto na ndio maana wakatoa vifaa ivyo kwa ajili ya kuwalinda ambapo alisema wanategemea vifaa hivyo vitasambazwa katika shule.
Ametaja vifaa walivyotoa ni pamoja na barokoa 500 N95 ,Gun themometre nne za kupima joto ,wamekabidhi box 20 za sabuni za maji ya kunawia mikono, middle’s Paddle hand wash-facilities 35 ,matanki ya kuhifadhia maji kwenye vifaa vya kunawia mikono 20 na Chlorine powder kilo 126.
Pia Chlorine tablets kilo tano za kuna vitakasa mikono makasha 24, PPE 63, gloves boxes 83, spika 3 kwa ajili ya matangazo ya kuelimisha juu ya corona, vipeperushi 144, vienye ujumbe wa kuelimisha juu ya corona pamoja na bronchure 200 na bango 1na Face shield 333.
Aidha amesema mbali na vifaa hivyo wamejikita katika kutoa elimu kwa njia ya bodaboda ambazo watatumia vipaza sauti kucheza sauti iliyorekodiwa na wataalamu wa afya juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona.
Sakafu amebainisha kuwa watutumia wataalamu wa Halmashauri kutoa elimu ya corona kwa wananchi na watapita kwenye vijiji na magari, kutembelea kaya kuelimisha watu juu ya namna ya kujikinga na Corona.
Theresia Mahongo Mkuu wa wilaya ya Karatu (kushoto) na Katibu tawala wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda wakikagua vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona juzi vilivyotolewa na Taasisi ya Community Aid and Social Education Empowerment (CSEE) ikiwemo spika kwa ajili ya kusaidia kuelisha wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha (picha na Woinde Shizza).
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment