UVUTAJI WA TUMBAKU UNA ATHARI KIUCHUMI WA MTU MMOJA MMOJA ANAYETUMIA | Tarimo Blog


Na WAMJW-Dodoma

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema Tanzania kama nchi nyingine za Kiafrika wavutaji wa tumbaku wako hatarini kuyumba kiuchumi na kupata magonjwa yasiyoambukizwa kama tahadhari hazitachukuliwa mapema.

Waziri Ummy amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa matumizi ya tumbaku kwa watu wazima wa mwaka 2018 nchini uliofanyika mapema leo katika Ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema utafiti huo umeonesha kuwa kwa wastani matumizi ya tumbaku kwa mtu mmoja kwa mwezi inagharimu Shilingi za Kitanzania 28,840/= fedha ambayo ingetosha kupunguza kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi kwa mtu mmoja mmoja kwa mwezi kwa asilimia 58 na umaskini wa kupindukia (mahitaji ya chakula) kwa mtu mmoja mmoja kwa mwezi kwa asilimia 85.

“Kwa kutumia taarifa za Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya binafsi kwa Tanzania Bara wa Mwaka 2017-18, fedha za kujikimu kwa ajili ya mahitaji ya msingi kwa mwezi kwa mtu mmoja ni Shilingi za Kitanzania 49,320/= na mahitaji ya chakula kwa mwezi kwa mtu mmoja ni Shilingi za Kitanzania 33,748/=”. Amesema Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa utafiti huo, Matokeo yameonesha kuwa mtu mmoja kati ya 10 (8.7%), wenye umri wa miaka 15 au zaidi nchini Tanzania wanatumia tumbaku ya aina yeyote na hivyo kuwa na watu milioni 2.6 kati ya watu zaidi ya milioni 55. Wanaume ni asilimia 14.6 na wanawake ni asilimia 3.2.

Aidha, Waziri Ummy amesema watu 4 kati ya 10 (40.3%) nchini wamewahi kuona onyo la matumizi ya tumbaku kupitia redio au runinga. Pia matokeo ya utafiti yameonesha kuwa, watu 9 kati ya 10 (92.3%) wenye umri wa miaka 15 au zaidi wanaamini uvutaji wa sigara husababisha magonjwa, wakati watu 8 kati ya 10 (84.4%) wanaamini kuvuta hewa ya mtu anaevuta sigara kunaweza kuwasababishia magonjwa hata kama wao hawavuti sigara.

katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Taarifa inaonesha kuwa watu 4 kati ya 10 (32.9%) wameathiriwa na moshi wa tumbaku sehemu za kazi ikiongozwa na sehemu za mabaa na kumbi za starehe kwa asilimia 77 (watu milioni 3), maeneo ya huduma za biashara za vyakula asilimia 31.1(watu milioni 3.5) na majumbani asilimia 13.8 (watu milioni 4.1).

Waziri Ummy amesema utafiti huo una umuhimu wa kipekee katika Wizara, kwani matokeo yake yatasaidia katika kutathmini hatua zilizofikiwa katika kupambana na magonjwa makuu manne yasiyoambukiza ambayo ni Saratani, magonjwa ya moyo, magonjwa ya mfumo wa hewa na kisukari.

katika kuhakikisha elimu dhidi ya athari ya tumbaku inaifikia jamii ipasavyo. Waziri Ummy ametoa maelekezo kwa Watendaji wa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na wadau wengine, kutengeneza au kupitia upya Sheria ya kudhibiti matumizi ya Tumbaku ili iendane na Mkataba wa Kimataifa wa kudhibiti matumizi ya Tumbaku na kuendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhusu madhara yake;

Wizara ya Elimu kuendelea kuimarisha juhudi za kuwakinga wanafunzi dhidi ya tumbaku na bidhaa zake; Wizara ya mambo ya ndani kuhakikisha wale wanaokiuka miongozo kama vile kuendelea kuvuta sigara kwenye maeneo ya wazi wanachukuliwa hatua stahiki; Watengenezaji na wauzaji wa sigara, kufuata miongozo iliyowekwa na Serikali ikiwemo kutokuweka mabango au kutangaza na kuhamasisha matumizi ya sigara, kupitia bidhaa kama miamvuli, T-Shirts, kofia, na kutowauzia watoto wenye umri chini ya miaka 18; jamii kuacha kutumia tumbaku na bidhaa zake na Taasisi za Utafiti kufanya Tafiti za kuangalia vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku ilikuwe na takwimu za nchi na siyo kutegemea za kutoka nje.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2