FREDRICK LOWASsA AIBUKA KINARA KURA ZA MAONI JIMBO LA MONDULI | Tarimo Blog

Na Jusline Marco-Arusha

Wajumbe wa mkutano mkuu Chama Cha Mapinduzi jimbo la Monduli mkoani Arusha wamemchagua Mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa Ndg: Fredrick Lowassa kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo kwa kupata kura 244 kati ya wapiga kura 582.

Akitangaza matokeo ya kura za maoni msimamizi wa uchaguzi huo Jasmin Bachu amesema kuwa matokeo hayo siyo ushindi wa kuwa ubunge bali ni mwanzo wa mchakato wa awali wa kufanikisha vikao vya uteuzi kuweza kuteua mgombea.

Aidha katika kinyang'anyiro hicho jumla ya wajumbe 582 waliweza kupiga kura hivyo kupelekea mgombea Julius Kalanga kupata kura 162 akifuatiwa na Wilson Lengima ambaye alipata kura 149 ambapo katika matokeo hayo kura moja iliweza kuharibika.

Hata hivyo wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi Wilayani Monduli kutoka katika  zaidi ya kata 18 wamehusika kufanya mchakato wa kura za maoni ambao umehusisha wagombea 24 huku ushindani ukionekana kwa wagombea wapatao 3 ambao ni aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Julius Kalanga,mwenyekiti wa ccm wilaya Wilson Lengima pamoja na mtoto wa aliyekuwa  waziri mkuu mstaafu Fredrick Lowassa.
 Fredrick Lowassa akisaini baada ya kuibuka kidedea katika mchakato wa kura za maoni Jimbo la Monduli,Mkoani Arusha
Kulia ni Fredrick Lowasa,katikati ni Wilson Lengima na kushoto ni Julius Karanga wakisubiri kuhesabu kura zao baada ya mchakato wa uchaguzi kukamilika.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2