Na Jusline Marco, Arusha
MTANDAO wa vikundi vya wakulima Tanzania kwa kushirikiana na Kisiwa cha amani cha Ubelgij (IDP) kwa pamoja wamezindua mradi wa kilimo Endelevu + wa miaka mitatu 2020 hadi 2023 uliolenga kuboresha usalama wa chakula na lishe,upatikanaji wa maji kwa wakulima katika familia za wafugaji Mkoani Arusha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema Serikali inahitaji kutambua shughuli zinazofanywa na wadau hao katika kufikia malengo ya kimaendeleo ya shughuli za kilimo na ufugaji zinazofanywa na jamii.
Kwitega amesema kuwa ni vyema malengo ya mradi huo yafanyike kwa wakati ili kutatua changamoto katika maeneo husika kwa manufaa ya binadamu na mifugo ambapo kutasaidia kuleta maendeleo kwa jamii nzima ya wakulima na wafugaji.
"Serikali inawajibu wa kutambua shughuli zinazofanywa na wadau mbalimbali wa kimaendeleo ikiwa na lengo la kusukuma maendeleo kwa jamii hivyo tuendelee na kazi hii ili tuweze kutatua changamoto katika maeneo yetu ndani ya mkoa huu," amesema Kwitega.
Kwa upande wa Meneja wa Mradi wa IDP, Ayesiga Buberwa amessema mradi huo utatekelezwa katika wilaya ya Karatu,Longido na Halmashauri ya Jiji la Arusha ikiwa ni matokeo ya awali ya upatikanaji wa maji kwa ajili ya kilimo ,mifugo na matumizi ya binadamu katika wilaya hizo ambapo umeboreshwa na kufikia kiwango kilichoridhisha.
Aidha ameongeza mradi huo umefadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Luxemberg na kutekelezwa na MVIWATA Arusha pamoja na RECODA katika Wilaya za Karatu na Longido vilevile katika halmashauri ya jiji Mkoani Arusha.
Ameeleza kuwa kupitia mchakato wa utoaji wa elimu na mafunzo kwa jamii,mashirika yashughulikayo na mifumo ya maji katika jamii,mradi huo utaongeza viwango vya uzalishaji na kubadilisha uzalishaji wa familia za wakulima ili kupunguza upungufu wa chakula,kuongeza kiwango cha mazao yanayozalishwa na kuuzwa na kutoa chakula bora kwa binadamu.
Wakati huo huo Mratibu wa Mradi huo Richard Masandika amesema kuwa mradi huo ambao utatekelezwa katika wilaya za Longido na Karatu utachukuwa nafasi ya kuendeleza miradi iliyokuwa ikitekelezwa kwenye maeneo mawili ambayo miradi ya awali ilikuwa imemaliza muda wake iliyokuwa ikishughulikia miungombinu ya maji chini ya maji kwa ajili ya mifugo na watu.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizindua mradi wa kilimo endelevu + ulioandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Arusha kwa kushirikiana na Kisiwa cha amani cha Ubelgiji (IDP) pamoja na RECODA
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kilimo Endelevu+,hafla iliyofanyika jijini Arusha chini ya ufadhili wa wizara ya mambo ya nje ya Luxemberg na kutekelezwa na MVIWATA Arusha pamoja na RECODA
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment