FREDRICK LOWASSA ASHINDA KURA ZA MAONI JIMBO LA MONDULI,WANANCHI WAMPONGEZA | Tarimo Blog


Na Pamela Mollel,Monduli

Mtoto wa aliyekuwa waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa Fredrick Lowassa, ameibuka mshindi katika uchaguzi wa kura za maoni za kumpata mgombea atakaepeperusha bendera ya ubunge kupitia CCM katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika October mwaka huu

Akitangaza matokeo hayo mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu maalum uliofanyika Wilayani Monduli Msimamizi wa uchaguzi John Nkini amesema Fredrick Lowassa ameshinda kwa kupata kura 244 kati ya kura 582 zilizopigwa

Aidha Mchuano katika uchaguzi huo ulikuwa mkali ambapo watia nia waliokuwa wakichuana kwa kasi ni Fredrick Lowasa aliyepata 244,Julius Kalanga kura 162 na Wilson ole Ngima kura 149

Nkini amewataja Watia nia kwa nafasi ya Ubunge katika uchaguzi huo kuwa walikuwa 24 huku wajumbe waliopiga kura ni 582 ambapo amesema kura moja imeharibika.
Wananchi wakishangilia huku gari la Fredrick Lowassa likitoka eneo la chuo cha Ualimu Monduli.

Fredrick Lowassa aliyevalia koti jeusi akihesabu kura zake Mara baada ya uchaguzi kufanyika huo kufanyika Wilayani Monduli

Fredrick Lowassa akiwa ameshikilia kura zake
Kushoto ni aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli Julius Kalanga akishikilia kura zake,pembeni Wilson Ole Ngima ambaye wamechuana vikali

Wajumbe wa mkutano Mkuu maalumu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Monduli wakifatilia uchaguzi

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2