RC mpya awasili Njombe,aomba ushirikiano | Tarimo Blog

 Marwa Mwita Rubirya mkuu mpya wa mkoa wa Njombe akizungumza na viongozi mbali mbali katika ofisi za mkoa wa Njombe mara baada ya kupokewa mkoani humo.
 Eng ,Marwa Mwita Rubirya mkuu mpya wa mkoa wa Njombe akiwasili katika ofisi za mkoa wa Njombe.
Eng, Marwa Mwita Rubirya mkuu mpya wa mkoa wa Njombe akisalimiana na baadhi ya viongozi mara baada ya kuwasili mkoani Njombe.

Na Amiri Kiligalila,Njombe
MKUU wa mkoa wa mpya wa Njombe Enjinia Marwa Mwita Rubirya aliyeteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais John Pombe Magufuli , amewasili kituo cha kazi na kuzungumza na baadhi ya watumishi wa mkoa na wilaya ya Njombe ambapo amesema atafanya ziara katika wilaya zote nne za mkoa wa Njombe huku akiomba ushirikiano kwa viongozi wa wilaya hizo.

Mara baada ya kuwasili katika ofisi za mkoa, mkuu huyo mpya amepokea taarifa kutoka kwa katibu tawala wa mkoa wa Njombe Bi,Catarina Revocat na mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri muda mfupi baada ya kukaribishwa.

“Wananchi wa Njombe ni wananchi wasikivu,wachapakazi na tunaamini utafanya nao kazi vizuri sana”. Alisema Catrina Revocat katibu tawala wa mkoa wa Njombe

Eng.Marwa Mwita Rubirya ameahidi kushirikiana na viongozi wa halmashauri mkoa na wilaya katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi vijijini.

“Nitategemea ushirikiano mkubwa kwa wenzangu hapa na ambao wako wilayani,najua taarifa itaandaliwa ili inisaidie kujifunza Njombe tunafanya nini na ni wapi tuongeze nguvu zaidi ili hatimaye tuwasaidie wananchi”alisema Eng.Marwa Mwita Rubirya 

Rubirya awali alikuwa meneja wakala wa barabara Tanzania (TANROD) mkoa wa Mwanza na amechukuwa nafasi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Njombe Cristopher Ole Sendeka aliyekwenda kwenye majukumu mengine ya kisiasa.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2