SERIKALI YATOA MSAMAHA WA KODI KWA MRADI WA UMEME GEITA - NYAKANAZI | Tarimo Blog

Kasi ya Utekelezaji Mradi Mkubwa wa Kusafirisha umeme katika msongo wa Kilovolti 220 wa Geita-Nyakanazi wenye urefu wa kilomita 144 na unaosimamiwa na TANESCO imezidi kuongezeka baada ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha kutoa msamaha rasmi wa kodi ambayo ni zaidi ya takriban bilioni 25.

Meneja wa mradi kutoka TANESCO, Mhandisi Olalo Sospeter amesema kuwa, hapo awali kazi za Mradi huo zilikuwa zikienda taratibu kwa kusuasua kutokana na mkandarasi kushindwa kuagiza ndani ya Nchi baadhi ya vifaa muhimu vya ujenzi wa mradi huo kutokana gharama za kodi ambazo kimkataba hazikutolewa na wafadhili wa Mradi huo.

Mradi unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya maendeleo ya Ujerumani (KFW), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na Umoja wa Ulaya (EU) kwa gharama za jumla ya Shilingi Bilioni 96 na Unatarajiwa kukamilika Mwezi Februari 2021.

Kukamilika kwa Mradi huo kutawezesha upatikanaji wa Umeme wa gridi ya taifa wa uhakika na wa gharama nafuu katika ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Nchi, hivyo kuipunguzia TANESCO na Serikali gharama kubwa ya kuzalisha umeme ghali wa mafuta Mazito ya Dizeli unaotumika katika Mikoa ya Kigoma na Wilaya za Mkoa wa Kagera kama vile Ngara na Biharamulo hivi sasa.

Aidha Meneja wa Mradi huo Mhandisi Olalo aliongeza kuwa, mradi huo wa kusafirisha umeme unakwenda sanjari na mradi kabambe wa kusambaza umeme kwa wannchi zaidi ya 10,000 wa awali katika vijiji 32 vilivyo pembezoni mwa maeneo ambayo yatapitiwa na mradi huo kuanzia Chato Geita, Biharamulo Kagera na Wilaya ya Kakonko Kigoma. 

Kukamilika kwa Mradi huo kunatarajiwa kufungua fursa za uwekezaji wa Miradi mikubwa ya kiuchumi na ile ya kimaendeleo ya kijamii kwa wananchi katika Ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Nchi ya Tanzania na maeneo ya jirani kwa ujumla ambayo hapo mwanzo uwekezaji mkubwa kwa gharama nafuu za uendeshaji ulishindikana kutokana na kutokuwepo umeme wa bei nafuu wa TANESCO.
 Ujenzi wa kituo kikubwa cha kupoza umeme cha Nyakanazi kilichopo eneo la nyakanazi Mkoani Kigoma ukiendelea.
 Meneja wa mradi wa Geita Nyakanazi toka TANESCO Mhandisi Sospeter Olalo

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2