*Ununuzi wa bidhaa za ndani ni kulinda ajira nchini
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikioa na Tawala za Mitaa (Tamisemi) Seleman Jaffo amesema kuwa fedha zinazoelekezawa katika Miradi ya Miundombinu ya ujenzi katika Halmashauri na Mikoa kuhakikisha wananunua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
Jaffo ameyasema hayo wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha vifaa vya Umme cha Africab kilichopo kurasini jijini Dar es Salaam , amesema kuwa kulinda viwanda vya ndani ni kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa zinapata soko la kutosha ikiwa pamoja na kulinda ajira zinazotolewa kwa wananchi katika viwanda hivyo.
Amesema Africab imewekeza katika vifaa vya umeme ambapo vinakidhi viwango hivyo hakuna sababau ya kununua biadhaa za nje wakati bidhaa za ndani zina vwango kuliko bidhaa za nje ya nchi.
Jaffo amesema kuwa watanzania kwa pamoja wakinunua bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani kutafanya wanaoagiza biadhaa hizo na kuanza kuagiza katika viwanda vya ndani hali ambayo itafanya viwanda kuongeza uzalishaji pamoja na ajira kuongezaka kwa wazawa.
"Tanzania sio nchi kuwa jalala kwa bidhaa zisizo na ubora na wananchi wanatakiwa kuwa walinzi wa bidhaa zinazolishwa katika viwanda vya ndani ,ulinzi wa bidhaa za ndani sio kutumia bunduki bali ni kukunua kuthamini bichaa zinazalishwa katika viwanda vya ndani"amesema Jaffo.
Aidha amesema Africab wameajiriri wafanyakazi 400 ambapo ni watanzania hivyo kuacha kununua bidhaa katika kiwanda hicho ni kutaka kupoteza ajira za wafanyakazi hao.
Amesema kuwa nchi kuingia uchumi wa kati ni pamoja na viwanda vilivyojengwa na vinavyoendelea kujengwa hivyo bidhaa zinazozalishwa ndani zitumike katika ujenzi wa vitu mbalimbali.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe amesema kuwa kauli ya Waziri wa Tamisemi kilichobaki ni utekelezaji tu katika miradi kwa wilaya ya Temeke kununua bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani.
Gondwe amesema kuwa Temeke imepata bahati ya kuwa na Kiwanda kikubwa cha vifaa vya umeme na vina ubora.
Afisa wa Masoko wa Kiwanda cha Africab, David Tarimo amesema kuwa wameanza uzalishaji miaka 19 walianza na kutengeneza nyaya za umeme lakini sasa wamekwenda mbali wanategeneza hadi mitambo ya kupoozea umeme.
Amesema kuwa ziara ya Waziri Jaffo inafungua milango ya kuafanya kuendelea kuzalisha zaidi kwa kupanua masoko
Tarimo amesema kuwa bidhaa hizo wanauza Afrika Kusini, Malawi, Zambia pamoja na Rwanda hivyo soko linahitajika zaidi kwa kwa uzalishaji unaanza wa kebo za umeme.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Tawala za Mitaa (Tamisemi) Seleman Jaffo akizungumza mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha vifaa vy umeme katika Kiwanda cha AfriCab jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe akizungumza kuhusiana na ziara ya Waziri Jaffo katika kiwanda cha African kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Africab Mansour Moizz akimpa maelezo namna wanavyozalisha bidhaa mbalimbali ndani ya kiwanda.
Mkurugenzi wa Africab Mansour Moizz akimpa maelezo namna wanavyozalisha bidhaa mbalimbali ndani ya kiwanda.
Afisa Masoko wa Africab David Tarimo akizungumza kuhusiana ziara ya Waziri Jaffo namna alipowapa moyo ya kuzalisha vifaa vya umeme.
Afisa Masoko Mkuu wa AfriCab Deo Rwakagera akiomuonesha Waziri Jaffo bidhaa za vifaa vya umeme zilizozalishwa na AfriCab.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment