WATAKAOBAINIKA KUTAFUNA FEDHA ZA TASAF KUCHUKULIWA SHERIA KALI | Tarimo Blog

WATAFUNAJI watakao bainika kufuja fedha za walio katika mpango wa TASAF kipindi cha pili cha Awamu ya  Tatu unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wameonywa kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Onyo hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF, (National Steering Committee )  Eng. Rogatus Mativila, wakati wa kufuatilia zoezi la Uhakiki lililoanza leo kwenye Kata sita (6) Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Matavila, amesema kuwa kumekuwepo na Walenga hewa sio jambo jema hata kidogo jambo ambalo limekuwa likitolewa malalamiko sana.

“Uwepo wa kaya hewa katika maeneo ya utekelezaji  aibu sana kwa viongozi wa mikoa, wilaya na Halmashauri.Serikali haitakuwa na huruma kwa mtu yeyote. Kufanikiwa ama kutofanikiwa kwenye maeneo yenu itakuwa mojawapo ya vipimo nnitakavyotumia kujua kama mastahili kuendelea na nafasi mlizonazo au la. Siwatishi lakini huo ndio ukweli’’ Amesema Mativila.

Amesema katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa, walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini watahakikiwa kwa kuondolewa au kuingizwa katika mpango kwa kufuata vigezo vilivyowekwa a serikali.

Mativila, amesema kuwa Uwajibikaji na uadilifu kwa wataalamu ni muhimu katika kusimamia zoezi la uhakiki wa Walengwa wa  Mpango wa TASAF ambao  utasaidia kupata Takwimu sahihi  za wanufaika Halisi  ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Amesema  kuwa, Mkazo mkubwa katika Kipindi cha Pili utawekwa katika kuwezesha Kaya zitakazoandikishwa kwenye Mpango kufanya kazi ili kuongeza kipato na kuhakikisha kwamba huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa  na kuendeleza rasilimali watoto hususani katika upatikanaji wa elimu na afya. 

Aidha, amesema Pamoja na hayo tathimini ya serikali ya utekelezaji wa TASAF kipindi cha kwanza awamu ya tatu inaonyesha umaskini nchini umepunngua kwa asilimia 10 kwa mahitaji ya msingi na umaskini uliokithiri umepungua kwa asilimia 12 kwa kaya maskini sana nchini.

 Amewasisitiza  Viongozi na Maafisa Waandikishaji Kaya kufanya kazi kwa uadilifu na weredi wakati wa utekelezaji wa Zoezi hili  kama maagizo yaliivyotolewa na Mh Rais katika hotuba  yake wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Pili kuhusu uwepo wa kaya hewa.

 “ Uwepo wa kaya hewa katika maeneo ya utekelezaji ni aibu sana kwa viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri. Nitoe wito kwa wahusika wote kusimamia vizuri mradi huu. Serikali haitakuwa na huruma kwa mtu yeyote. Kufanikiwa ama kutofanikiwa kwenye maeneo yenu itakuwa mojawapo ya vipimo nitakavyotumia kujua kama mnastahili kuendelea na nafasi mlizonazo au la. Siwatishi lakini huo ndio ukweli.” Amesema Mativila

Hata hivyo amewakumbusha  wananchi wote kuchukua tahadhari ya ugonjwa hatari wa COVID-19  ili   kuepuka Mikusanyiko isiyoyalazima, kuvaa barakoa,  kuepuka kushikana  mikono na  kunawa mikono kwa sabuni kwa kutumia maji safi yanayotiririka pamoja na kutumia vitakasa mikono.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2