WATU 15 WANAOTUMAGA UJUMBE WA KUDAI WAMEKOSEA KUTUMA FEDHA KWENYE SIMU WAFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU | Tarimo Blog



Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

WAKAZI 15 wa Ifakara wanaodaiwa kutuma ujumbe mbalimbali za kukosewa kutuma fedha wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na kesi ya mtandao kula njama ya kutenda kosa na kusambaza ujumbe bila ridhaa ya mmiliki wa simu.

Pia wanatuhumiwa  kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, pamoja na kutumia namba za simu zilizosajiliwa na Mtu mwingine ikiwemo kutuma ujumbe kuonyesha umepokea kiasi cha Pesa.

Washtakiwa hao wamefikishwa mbele ya mahakimu watano tofauti ambao ni Hakimu Mkazi Mwandamizi  Augustina Mmbando, Hakimu Mkazi Mwandamizi,  Rashid Chaungu, Hakimu Mkazi Mkuu Richard Kabate, Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi na Hakimu Mkazi Mkuu Yusto Ruboroga.

Wanaoshtakiwa ni Rashid Mshamu (23) ambaye ni dereva Pikipiki na Emmanuel Assey (19) Wakala wamefikishwa mbele ya Hakimu Chaungu ambapo wanakabiliwa na mashitaka sita.Wamedaiwa walilitenda kosa hilo kati ya Januari 1 na Juni 15, 2020 Kilombero mkoani Morogoro ambapo walikuwa njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Imedaiwa mshtakiwa Mshamu  anadaiwa kusambaza taarifa za uongo kati ya Januari Mosi na Juni 15, 2020, Ifakara mkoani Morogoro kwa lengo la kulaghai alituma ujumbe wenye taarifa za uongo.

Pia wanadaiwa kuchapisha taarifa za uongo kosa wanalodaiwaqq kulitenda Aprili 15, 2020 Ifakara Morogoro ambapo walituma ujumbe kwa mfumo wa Kompyuta wakisema "Imethibitishwa umepokea 170,000" kutoka kwa Adamson Cheyo na kusema salio lako ni 430,000"
 
Washtakiwa hao wanadaiwa kushindwa kutoa taarifa za mabadiliko ya kadi simu, ambapo wanadaiwa wametenda kosa hilo Januari 1, 2020 na Juni 15, 2020 Kilombero, mkoa Morogoro"

Wakati kosa jingine la matumizi mabaya ya taarifa linamkabili mshitakiwa Assey ambapo anadaiwa kati ya Januari Mosi na Mei 30, 2020 Ifakara Morogoro akiwa Wakala wa  huduma za kifedha za mitandao ya simu kwa alitumia namba mbalimbali za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine.

Pia wanatuhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo wanadaiwa kulitenda Januari 1 na Juni 15, 2020 katika maeneo tofauti mkoani Morogoro ambapo kwa nia ovu walijipatia Sh milioni tatu  wakidai fedha hizo zimetumwa kwa watu kimakosa.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 27,2020 kwa ajili ya kutajwa.

Mbele ya Hakimu Ruboroga washitakiwa  Saidi Sevenjari maarufu Dangote (35) mkulima na Hasani Njalatango 34 mkulima walisomewa mashitaka sita.

Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori amedai kati ya Januari Mosi na Juni 15, 2020 maeneo mbalimbali wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro washitakiwa Sevenjari na Njalatango kwa pamoja walikula njama kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Pia mshtakiwa Sevenjari,  anadaiwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi alituma ujumbe ukionesha Airtel money  namba umepokea Sh 300,000 kutoka kwa Antony Ngonyani mnamo Juni 22 mwaka huu saa mbili asubuhi salio lale lake ni sh. 750,000.

Dangote anadaiwa alijipatia Sh  2,132,980 kutoka namba mbalimbali kwa kudanganya kwamba fedha hizo zimetumwa kimakosa arudishiwe.

Nyantori amedai Mei 22 mwaka huu maeneo ya Ifakara kwa kupitia mfumo wa Kompyuta mshitakiwa huyo alisambaza ujumbe kuonesha Ngonyani alipokea Sh 300,000 na salio lake ni 750,000 na kwamba fedha hizo zimetumwa kimakosa hivyo, arudishiwe.

Pia wanadaiwa , kati ya Januari Mosi  na Juni 15 mwaka huu maeneo mbalimbali ya Kilombero, walitumia namba za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine bila kutoa taarifa kwa mtoa huduma.

Washitakiwa wamekana mashitaka wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana  ya kuwa na wadhamini wawili wenye barua, watakaosaini kulipa Sh  milioni tano Kesi hiyo itatajwa, Agosti 5 mwaka huu.


Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya Hakimu Shaidi na Wakili wa Serikali, Batilda Mushi imedai kuwa washitakiwa Ndiu, Likumbai, Migoi,Tojo na Ngejela wanadaiwa, kati ya Januari 2,2020 na Juni 10,2020 wilayani Kilombero mkoani Morogoro, walikula njama kutenda kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Katika mashitaka ya kusambaza ujumbe wa kielektroniki inadaiwa Ndiu, Likumbai, Migoi walianzisha ujumbe wa mtandao kuonesha Ashura Birika amepokea Sh 150,000 Aprili Mosi, 2020 saa 3:03 asubuhi na salio lake ni Sh 230,000.

Ngejela anadaiwa kujipatia Sh. 316,683 kutoka kwa watu tofauti akidanganya kuwa fedha zimetumwa kwao kimakosa hivyo arudishiwe na kwamba mshitakiwa Ndiu alijipatia Sh 1,633,219 kutoka kwa watu tofauti akidanganya fedha zimetumwa kimakosa.

Pia Mushi amedai Aprili Mosi, 2020 mshitakiwa Ndiu, Likumbai na Migoi walitoa taarifa za uongo kwa kutumia mtandao kuonesha Sh 150,000 zilitumwa kwa Birika  na kwamba salio lake ni 320,000.

Katika mashtaka ya matumizi mabaya ya taarifa, inadaiwa Tojo na Ngejela akiwa Wakala wa watoa huduma za simu alitumia taarifa za wateja vibaya kwa kuuza laini za simu zilizosajiliwa na watu wengine.

Mshtakiwa Ndiu na Likumbai na Migoi wanadaiwa  kutumia namba zilizosajiliwa kwa majina mengine bila kumtaarifu mtoa huduma.

Washitakiwa wamekana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai upelelezi umekamilika hivyo aliomba tarehe nyingine ya kusikiliza maelezo ya awali.

Hakimu Shaidi aliwataka kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho na barua watakaosaini bondi ya Sh milioni mbili.mwishoooo

Mbele ya Hakimu Kabate, mfanyabiashara Filbert Ngatunga (26), Octavian Lekaleka (26) mfanyabiashara Francis Mhombera (24), Moses Mhindi (25) dereva bodaboda walisomewa mashtaka yao huku washtakiwa
Michael Ngalami (21) Omary Mbena (31) Wakala  ambao wamesomewa mashtaka saba mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustina Mbando.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2