Benki Ya NBC Yachangia Mil 114.7 Kuboresha Elimu Na Kilimo Mkoani Simiyu | Tarimo Blog

 Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa fedha kiasi cha Sh 114.7 Milioni kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya Kilimo na Elimu mkoani Simiyu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kuunga mkono jitihada za serikali katika kuendeleza sekta hizo muhimu.
Akipokea mchango huo kwenye hafla maalum iliyofanyika kwenye Maonesho ya Kilimo ya NaneNane  yanayofanyika kitaifa, mkoani  Simiyu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka pamoja na kuipongeza benki hiyo ameelekeza sehemu ya fedha hiyo itumike kujenga kisima cha Shule ya Sekondari ya wasichana Maswa na kuandaa shamba la hekali 50 litakalokuwa na alama ya benki hiyo.
“Kwa kuwa benki ya NBC imekuwa mstari wa mbele katika kutusaidia hasa katika masuala yanayoacha alama kama haya ya ujenzi wa miundombinu ya elimu na sekta ya kilimo na sisi kama mkoa tumeona ipo haja ya kutambua mchango huo kwa kuwapatia heshima hiyo wanayostahili,’’ alisema
Aliipongeza benki hiyo kwa kuteuliwa kuwania tuzo uzo za ubora za Afrika katika kuwahudumia wajasiliamali ambazo zinaakisi ufanisi wa benki hiyo katika kutoa huduma  za kibenki na kifedha katika bara la Afrika.
“Ni heshima kubwa kwa benki ya NBC na taifa kwa ujumla kuingia kwenye orodha ya benki tano bora zinazowania tuzo ya Benki Bora ya mwaka ya Wajasiliamali (SME Bank of the year) miongoni mwa benki zaidi ya 200, hatua muhimu zaidi kufikiwa na benki ya Kitanzania ndani ya mwaka huu.’’ alibainisha
Akitoa mchanganuo wa fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NBC Bw Theobald Sabi  alisema kiasi cha Shilingi milioni 40 ni udhamini wa benki hiyo kwenye maonesho hayo ya kilimo huku kiasi cha Shilingi milioni 10 kikilenga kuchangia ujenzi wa shule ya Sekondari ya Simiyu ambapo kitatosha kugharamia mifuko ya 541 ya saruji.
“Aidha kiasi cha milioni 19.9 kitakwenda katika kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari ya Anthony Mtaka ambapo kiasi hicho kitatosha kununua mifuko ya saruji 1080 na kiasi cha Shilingi milioni 44.8 kitatumika kugharamia uchimbaji wa kisima cha umwagiliaji wa mashamba ya viazi kwa vikundi vya akina mama wilayani Maswa.’’ Alisema.
Bw Sabi aliitaja baadhi ya jitihada za benki hiyo katika kuwahudimia wajasiliamali na wakulima kuwa ni pamoja na uendeshaji wa mafunzo maalumu ya kilimo na biashara kwa kushirikiana na Jumuiya wa Jumuiya wa Wafanyabiashara wanawake na Vijana (TABWA) pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE)yanayofanyika kwenye maonesho hayo.
“Pia tumekuja na huduma mahususi kwa ajili ya wakulima inayofahamika kama NBC Shambani inayolenga kuwasaidia wadau wa kilimo kutimiza malengo yao ya biashara ya kilimo ambapo inatoa fursa kwao kuwa na akaunti ya  vikundi vya wakulima kama vile AMCOS na vikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja,’’ alisema.
Alisema akaunti hiyo inawawezesha wakulima,wafugaji na wavuvi kufurahia huduma za benki hiyo bila kukatwa gharama zozote za uendeshaji kwani haina makato,na mtumiaji atakapofikisha pesa kuanzia laki moja atapatiwa faida kupitia riba.
“Ni jitihada kama hizi kwenye kilimo pamoja na kuwasaidia wajasiliamali kupitia vilabu vyetu vya kibenki ndio vimetuwezesha Benki ya NBC kuteuliwa ili   kuwania tuzo za ubora za Afrika katika kuwahudumia wajasiliamali ambazo zinaakisi ufanisi wa huduma  za kibenki na kifedha katika bara la Afrika.’’ Alisema.
Hafla hiyo ilihudhuliwa na baadhi ya viongozi wa serikali na wadau mbalimbali wa kilimo kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka (Kulia) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh Mil 19.9 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NBC Bw Theobald Sabi ikiwa ni sehemu ya fedha kiasi cha Sh Mil 114.7 ambacho benki hiyo ilitoa kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya Kilimo na Elimu mkoani Simiyu wakati wa hafla jioni iliyofanyika iliyofanyika kwenye Maonesho ya Kilimo ya NaneNane  yaliyofanyika kitaifa, mkoani  Simiyu
Waziri wa Kilimo Bw Japhet Hasunga (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NBC Bw Theobald Sabi ikiwa ni utambuzi wa benki hiyo kama mdhamini mkuu wa Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yaliyomalizika hivi karibuni mkoani Simiyu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NBC Bw Theobald Sabi akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau muhimu kwenye hafla hiyo akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Simity Bi Miriam Mmbaga (wa pili kushoto), Meneja Uhusiano wa benki hiyo Bw William Kallaghe (wa pili kulia),  mdau wa kilimo na msanii  Emanuel Mgaya maarufu kwa jina la Masanja (Kulia) na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Elias Barnabas (Kushoto)

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mwanza Bw Rodgers Masolwa akiwa ameshikilia tuzo ya utambuzi wa benki hiyo kama mdhamini mkuu wa Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yaliyomalizika hivi karibuni mkoani Simiyu. 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Elias Barnabas akitoa burudani kwenye hafla hiyo.

Mdau wa kilimo na msanii wa injili, Emanuel Mgaya maarufu kwa jina la Masanja akitoa burudani wakati wa hafla hiyo.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2