CHANGES YAWAKUTANISHA ZUCHU NA SHO MADJOZI | Tarimo Blog

DJ wa wasafi Rommy  Jones a.k.a Rj the dj akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutambulisha Albamu ya 'CHANGES' hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam leo. 

    Al-Hassan Muhidin, Michuzi Tv
DJ wa wasafi Rommy  Jones a.k.a Rj the dj  ametambulisha Album yake inayokwenda kwa jina la 'CHANGES'.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa albamu hiyo katika Hoteli ya  Hyatt Regency jijini Dar es salaam Rommy amesema katika albamu hiyo yeye hajaimba.

"Sijashiriki kwenye kuimba ila nimejaribu kukutanisha wasanii kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania,"

Miongoni mwa walioshirikishwa kwenye albamu hiyo ni pamoja na Morgan heritage, Sho madjozi kutoka Afrika Kusini, Mbosso pamoja na mwanadada Zuchu kutoka kundi la Wasafi (WCB).

 Aidha,Rommy amesema ndani ya Albamu hiyo kuna ladha tofauti tofauti za Muziki.

Hata hivyo ametangaza Agosti 16  itakua siku rasmi kuzinduzi albamu hiyo. 

Pia amesema angependa kualika baadhi ya wasanii wa nje ila kutokana na janga la Covid 19 limesababisha kutokuepo kwao kutokana na nchi zao bado zipo kwenye Lockdown.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2