KUSAYA ABAINI KIWANDA CHA MBOLEA KISICHO NA USAJILI WA UBORA | Tarimo Blog


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiwa ameshika chupa ya mbolea inayozalishwa na kiwanda cha Isacha Feeder cha Moshi leo alipokagua .Katika ziara hiyo alibaini kuwa kiwanda hicho kinazalisha mbolea ya maji aina ya Booster II ambayo haijasajiliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na  ameagiza mmiliki wa kiwanda hicho aende Dodoma ifikiapo 03 Septemba kujieleza kwanini anaendesha kiwanda bila usajili.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya( kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) Dkt.Stephano Ngailo wa kwanza kushoto alipobaini mbolea ya maji isiyo uthibitisho wa ubora toka TBS .Wa kwanza kushoto ni Msimamizi wa kiwanda cha Isacha Feeder -Njoro chaMoshi  Rajab Issa Juma kinachozalisha mbolea hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( kulia) akikagua mgodi wa chokaa (limestone rock)  leo alipotembelea kiwanda cha mbolea cha ABM Jijini Tanga.Kushoto ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Aubray Maimu.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (kulia) akiangalia eneo panapochimbwa chokaa kilimo katika kiwanda cha mbolea cha ABM Tanga. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania Bw.Saad Kambona.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiwa anatazama jiwe la chokaa linalotumika kuzalisha mbolea katika kiwanda cha ABM Tanga leo alipotembelea kukagua utendaji kazi wake na kuhamasisha kuongeza uzalishaji ili wakulima wapate mbolea kwa gharama nafuu.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( wa tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Bodi ya Mkonge Tanzania na wanahabari mara baada ya kutembelea bodi hiyo leo jijini Tanga kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya  Waziri Mkuu.
(Picha na habari na Wizara ya Kilimo)
 ……………………………………………………………
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesikitishwa na kitendocha kiwanda cha mbolea za maji cha Isacha Feeders Intertrade cha Moshimkoani Kilimanjaro kuzalisha bidhaa za mbolea ambazo hazisajiliwa nakuthibitishwa ubora wake kwa wakulima.Akiwa katika ziara ya kukagua viwanda vya mbolea nchini leo Katibu Mkuu huyo alijionea bidhaa za mbolea ya maji iitwayo “Booster II”ikiwa katika ghala la kiwanda cha Isacha Feeder –Njoro Manispaa yaMoshi na kubaini kuwa haijasajiliwa na mamlaka za uthibiti ubora nchini.“Sijafurahishwa na utendaji kazi wa kiwanda hiki cha mbolea cha IsachaFeeders kuona mbolea inayozalishwa haijasajiliwa na Shirika la Viwango(TBS ) pia haina Barcode hali inayohatarisha mazao ya wakulima na afyaza walaji” alisema Kusaya.Taarifa ya kiwanda hicho cha mbolea ya maji imeonyesha kilianzishwamwaka 2016 kikizalisha mbolea ya maji ambazo zinauzwa kwenye madukambalimbali nchini bila kuwa na usajili wa ubora toka TBS.Kufuatia hali hiyo, Katibu Mkuu Kusaya ameagiza wamiliki wa kiwandahicho kwenda ofisini kwake Dodoma ifikapo tarehe 03 Septemba 2020 ilikujieleza kwanini serikali isichukue hatua za kukifunga kiwanda hicho hadiwakamilishe taratibu za usajili ili kulinda wakulima na uharibifu unaowezakujitokeza endapo mbolea hiyo ikikosa ubora.“Ninyi mnazalisha mbolea na kuipeleka kwa wakulima wangu sasa ikitokeamazao ya wakulima yameharibika na mbolea hii isiyo na uthibitisho waubora nani atalipia gharama hizo?” alihoji Katibu Mkuu KusayaKufuatia hali hiyo Kusaya alitoa maagizo matano kwanza, mmiliki wakiwanda hicho cha Isacha kuwasilisha taarifa inayoonyesha tangu mwaka2016 wamezalisha kiasi gani cha mbolea na wameuza wapi, piliwawasilishe uthibitisho wa cheti cha kuendesha kiwanda toka BRELA naShirika la Viwango Tanzania (TBS).Agizo la tatu mmiliki wa kiwanda mbolea cha Isacha aeleze kwaninikiwanda hakina bango la utambulisho na hakijulikani na uongozi wa mkoa
wa Kilimanjaro mahala kilipo na nne kiwanda hicho kiwasilishe taarifa yaulipaji kodi serikalini tangu kilipoanza kazi mwaka 2016 hadi sasa.“Mkija Dodoma nataka mje na taarifa kamili kuhusu uhalali wa kiwanda hikikuwa na sifa za kuzalisha mbolea inayokwenda kutumika na wakulima ilikuishawishi serikali kuwa mnastahili kuendelea ka kazi ” alisisitiza Kusaya.Kusaya alisema akirejea Dodoma atawaalika Wizara ya Viwanda naBiashara, Mamlaka ya Mapato (TRA) Shirika la Viwango (TBS), BRELA naMamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) wajadili hatua za kuchukua dhidiya viwanda ambavyo vinakiuka taratibu za uzalishaji mbolea nchini.Naye Msimamizi wa kiwanda hicho cha Isacha Feeder -Njoro, Rajab IssaJuma alisema kiwanda hicho kinazalisha lita 17,000 za mbolea ya maji(Booster II: Foliar Fertilizer for Use in all Crops) kwa mwaka ambapo litamoja huuzwa kwa bei ya shilingi 2,000 kwa wakulima.Awali Katibu Mkuu huyo alitembelea kiwanda cha mbolea ABM cha Tangakuona hali ya uzalishaji na kukuta kiwanda hicho kikizalisha chokaa kilimochini ya uwezo wake kutokana na changamoto ya mtaji.Akizungumza na waandishi wa habari kiwandani hapo Mkurugenzi wakiwanda hicho Aubray Maimu alisema wanazalisha tani 5,000 za chokaakilimo (limestone) kati ya lengo la tani 10,005 kufikia mwaka 2021.“Mgodi wetu wa Zange Mkulumuzi hapa Kange Tanga una mawe yachokaa zaidi ya tani milioni 25 inayotesheleza uzalishaji wa mbolea yachokaa kwa wakulima” alisema Maimu.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Udhibiti wa MboleaTanzania (TFRA) Dkt. Stephano Ngailo amesema mahitaji ya mboleanchini ni tani 664,000 wakati uzalishaji katika viwanda vyote 12 umefikiatani 38,000 pekee kwa mwaka.Katibu Mkuu Kusaya yuko katika ziara ya kukagua na kujionea hali ilivyokwenye viwanda vya mbolea nchini ambapo tayari ametembelea kiwandacha Mbolea za Asili cha Guavay cha Dar es Salaam ambapo anatarajiakutembelea pia mikoa ya Arusha na ManyaraLengo la ziara hii ni kuhamasisha wawekezaji wa ndani ya nchi na njekuanzisha viwanda vya mbolea ili wakulima wapate kwa gharama nafuu nakaribu na mashamba yao badala ya kutegemea mbolea toka nje.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2