WADAU WAJADILI NAMNA YA KUKABILIANA NA USUGU WA DAWA ZA KUTIBU UKIMWI | Tarimo Blog

Mtafiti wa tafiti mbalimbali  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Kishiriki(MUHAS), Profesa Japhet Killewo akizungumza leo wakati wa kujadili mradi wa kujua usugu wa Dawa za Kutibu Ukimwi. Ikiwa wadau kutoka ChuoKikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa wakishirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi (MUHAS)  na  Chuo Ku lueven cha  nchini Ubelgiji walikaa na kujadili namna ya kukabilia na  usugu wa dawa za kutibu Ukimwi.

CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa wakishirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi (MUHAS)  na  Chuo Ku lueven cha  nchini Ubelgiji wajadili namna yakujua  usugu wa dawa za kutibu ugonjwa wa Ukimwi hapa nchini. 

Akizungumza na Michuzi Blog, Mtafiti wa tafiti mbalimbali  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Kishiriki(MUHAS),Profesa Japhet Killewo amesema mradi huo utasaidia kugundua namna dawa za Ukimwi zinavoleta usugu kwa watumiaji wa dawa hizo.

"Mradi wa Unaoshugulikia Usugu wa dawa za kutibu Ugonjwa wa Ukimwi hapa nchini utasaidia kuondoa usugu katika dawa pamoja na kuangalia nini kinasababisha kuwepo usugu katika dawa." Anesema Profesa Killewo

Hata hivyo amesema kuwa mradi huu unafanyika Ukonga na Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambako kuna watu zaidi ya Laki moja ambao wapo katika utafiti wa  usugu wa dawa za Ukimwi. 

Aidha Profesa Killewo amesema kuwa lengo la Mradi huo ni kuangalia wale ambao wameathirika na virusi vya Ukimwi kwani kati yao kuna ambao wanapewa dawa lakini haziwatibu.

  "Kwasababu dawa haziwatibu sababu zimepata usugu sisi tunataka kuangalia sasa kunausugu kiasi gani? Ili tuweze kuishauri serikali ili iweze kuangalia namna ya kutatua usugu wa dawa kwa watu waliothirika na virusi vya ukimwi ili wagonjwa waweze kubadilishiwa dawa hizo." Amesema Profesa Killewo

Mradi huo endapo ukifanikiwa nchi itafaidika kwa kujua ni watu wangapi wanatumia dawa na hawaponi na takwimu zitakuwa wazi na kuelewa namna ya kutatua changamoto hiyo na kupewa dawa ambazo zitawatibu waathirika wanaotumia dawa  zenye usugu.

Inasemekana kwa usugu upo tayari hapa nchini na  inakisiwa kuwa  ni zaidi ya  asilimia 30, hii ni sawa na watu 10  wanaopata dawa kati yao watatu wanatumia na haziwasaidii.

Hivyo Profesa Killewo amesema kuwa Utafiti huo utasaidia kuwajua watu wanaotumia dawa na haziwasaidii.
 Mratibu wa Mradi wa kuangalia usugu wa Dawa zenye usugu katika kutibu ugonjwa wa Ukimwi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dkt. Omary Swalehe akizungumza  jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya Wadau wakijadili Mradi wa usugu wa Dawa za Kutibu Ugonjwa wa Ukimwi.
 Baadhi ya wadau kutoko sehemu mbalimbali wakishirikiana na wadau wa jijini Dar es Salaam kujadili Mradi wa Usugu wa Dawa za Kutibu Ugonjwa wa Ukimwi wakionekana kushiriki Mkutano kwa Kupitia Video ( Zoom Conference).


Wadau wakifatilia Mkutano.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2