LATRA YAWATAKA WANANCHI KUANDIKA KWA MAANDISHI MAONI YA NDANI YA SIKU SABA KUHUSU NAULI ELEKEZI YA USAFIRI WA TRENI ARUSHA KWENDA KILIMANJARO | Tarimo Blog

Na, Jusline Marco;Arusha

MKURUGENZI Mkuu LATRA Gilliard Ngewe amewataka wananchi kuandika kwa maandishi maoni yao ndani ya siku saba na kuyawakilisha kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini kabla ya Septemba mwaka huu li yawe sehemu ya mchakato wa kutambua mapendekezo ya TRC kuhusu nauli zilizopendekezwa  kwa usafiri wa treni wa Arusha kwenda Moshi.

Ngwewe ameyasema hayo katika mkutano wa wadau wa treni ya abiria ya Arusha kwenda Moshi uliofanyika jijini Arusha ambapo amesema kila mwananchi amepewa nafasi ya kutoa maoni yake kuhusu  nauli elekezi itakayotumika katika usafiri wa treni.

Aidha amesema kuwa mkutano huo ni mahususi kwa ajili ya kukusanya mapendekezo kutoka katika shirika la reli Tanzania linalotaka nauli za huduma ya usafiri kwa abiria kuyoka Arusha kwenda Moshi pamoja na wadau wa usafiri huo kutoa maoni mapendekezo yao ili kwa pamoja waweze kuweka bei ya nauli ambayo itakuwa nafuu kwa kila mmoja.

Awali akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema takribani miaka 30 imepita usafiri wa treni ulisitisha safari zake hivyo ni wakati sasa kuchangamkia fursa ya usafiri huo kwani utakuwa rahisi na bei nafuu kwa mtanzania.

Kwa upande wao wadau wa usafiri wa treni Mkoani Arusha wameliomba Shirika la Reli Tanzania kuboresha bei za nauli katika kila daraja ili kumfikia kila moja kwenye usafiri huo sambamba na kuwajali watu wenye mahitaji maalum.

Akizungumza kwa niaba ya wadau hao Mwenyekiti wa wasafirishaji Mkoa wa Arusha Adolfu Massawe amesema ujio wa treni hiyo utarahisisha usafirishaji wa mizigo kwa wafanyabiashara watakao tumia usafiri huo na kufanya kufanya biashara kwenda vizuri pia hautaathiri usafiri wa magari ya abiria kwani njia zipo nyingi tofauti na njia ya treni ambayo iko moja tu.

Wakati huo huo Amina Njoka ambaye ni Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa Arusha amesema kama wamachinga wamefurahishwa na ujio wa usafiri huo kwani umesahisisha gharama za uletaji wa bidhaa zao ambapo amewataka wajasiriamali wadogo wafanyabiashara wadogo kutumia fursa hiyo katika kusafiri na kufuata mizigo yao sehemu mbalimbali.

Akizungumzia ushirikishwaji wa upangaji wa bei za nauli Amina amesema kuwa ni muafaka mzuri kwa wafanyabiashara kushirikishwa katika upangaji wa nauli kwani wanafahamiana wao kwa wao kutokana na mitaji yao kwani kabla ya ujio wa treni hiyo walikuwa wanakutana na changamoto mbalimbali ikiwemo gharama kubwa za nauli kutoka elfu 35 kwa basi hadi elfu 18 kwa treni.

Pamoja na hayo  TRC imetoa maoni yao kuhusu  mapendekezo ya nauli kwa abiria ambayo nauli kwa watu wazima kwa daraja la pili itakuwa shilingi elfu 2000,daraja la tatu shilingi elfu 1500 huku watoto ikiwa shilingi 400.

Ambapo kwa upande wa wadau hao wametoa mapendekezo juu ya bei za nauli ambapo wameomba kwa daraja wa tatu iwe shilingi elfu 1500 kwa watu wazima, daraja la pili shilingi elfu 2000 na upande wa watoto hususani wanafunzi kuwa shilingi mia 300 ambapo wameomba miziho yao kutochajiwa pindi wanaporipoti mashuleni na kurejea majumbani.

Sambamba na hayo kaimu katibu mtendaji kutoka baraza la ushauri la utumiaji wa usafiri wa ardhi LATRA CC Bi.Fatuma Kulita ametoa maoni juu ya mindombini ya shirika la reli kuzingatia matakwa ya abiria ili kuweka ushindani na usafiri wa mabasi na kupata wateja kwa wingi.
 Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega akifungua mkutano wa wadau wa Treni ya abiria Moshi-Arusha
Kaimu katibu mtendaji Fatuma Kulita kutoka Baraza la ushauri la utumiaji wa usafiri wa ardhi LATRA CCC akiwasilisha maoni na mapendekezo ya bei kwa wasafiri  wa treni katika mkutano wa wadau wa treni ya abiria ya Moshi - Arusha  uliofanyika jijini Arusha.
 Wadau wa Treni ya abiria ya Moshi - Arusha wakiwa katika mkutano wa kujadili na kupendekeza bei za nauli, mkutano uliofanyika jijini Arusha


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2