Picha ya Pamoja.
Na Farida Saidy, Morogoro
INAKADIRIWA kuwa mwaka 2020 zaidi ya watoto 440,000 walio chini ya umri wa miezi 0 hadi miezi 5 wataathirika na utapiamlo mkali licha kuwepo kwa viashiria vya kupungua kwa udumavu kwa watoto walio chini ya miaka mitano.
Haya yamesemwa leo Agosti 28, 2020 na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara hiyo, Edward Mbanga wakati akizindua mradi wa kutengeneza vyakula vya nyongeza kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5
Mbanga amesema idadi ya watoto waliodumaa imeongezeka kutoka milioni 2.7 mwaka 2014 hadi kufikia milioni 3 mwaka 2018 kutokana na ongezeko la jumla ya idadi ya watu
“Ulishaji sahihi wa watoto wakiwemo watoto wachanga umekuwa chini sana, ambapo mnamo mwaka 2018, asilimia 58 ya watoto wachanga wenye umri wa miezi 0-5 waliripotiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee, asilimia 35 ya watoto wenye umri wa miezi 6-23 walipatiwa vyakula mchanganyiko kwa kiasi kidogo na asilimia 30 walipata kiwango cha chini cha chakula kilichokidhi mahitaji ya mtoto.”
Mkurugenzi huyo ameendelea kusema kuwa katika kupambana na utapiamlo Serikali imekuwa ikitekeleza mpango mkakati wa Kitaifa wa Lishe ulioanza mwaka 2016 na unatarajia kufikia tamati 2021 ambao umejikita katika kuhakikisha watoto, wanawake, na wanaume wanapata lishe bora na kuondoa utapiamlo, ukondefu na udumavu
Akitoa wasilisho lake katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. German Leyna amesema pamoja na kuwa Tanzania imeonyesha mafanikio katika jitihada za kuondoa udumavu, ukondefu na uzito uliopungua bado haijafikia malengo ya kidunia
Akitoa salamu za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa niaba ya Makamu Mkuu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda, Naibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala amesema SUA itashirikiana na Serikali katika kuhakikisha mradi huo unafanikiwa
Katika Mradi huo SUA kupitia Idara ya Teknolojia ya Chakula, Lishe na Sayansi za Walaji inatarajiwa kutengeneza vyakula hivyo vya nyongeza kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment