MAAFISA 16 WASTAAFU WA JESHI WAPIGIWA GWARIDE MAALUMU LA HESHIMA JIJINI DAR LEO | Tarimo Blog

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
MAAFISA 16 wakuu wa jeshi hapa nchini wamekagua gwalide maalumu la heshima kwaajili ya kuaga baada ya kustaafu jeshi.

Viongozi hao wa juu ni Luteni Jenerali mmoja, Mameja Jenerali sita na Mabregedia Jenerali tisa wamekagua gwalide la heshima katika viwanja vya Twalipo Mgulani jijini Dar es Salaam leo.

Jeshi  liliwapa muda wa dakika 10 kwa kila mmoja kukagua gwaride maalumu la heshima baada ya kutumika jeshi hapa nchini kwa muda mrefu na kustaafu wakiwa buheri wa afya njema.

Akizungumza baada ya kupigiwa gwaride maalumu la heshima la jeshi, Brigedia Jenerali (mstaafu), Mery Hiki ambaye ametumika jeshi kwa miaka 45  amesema kuwa jeshi hapa nchini linataratibu zake ambazo mtu yeyote akizifuata ataishi Muda mrefu.

"Mimi kilichonifanya niishi miaka mingi jeshini ni kufuata taratibu na misingi ambayo imewekwa na jeshi na kusikiliza viongozi wangu, wakuu wangu na kuwa mnyenyekevu hiyo ndio siri yangu ya kuishi jeshini miaka mingi na kufikia mpaka kustafu nikiwa jeshini."
Amesema Brigedia Jenerali Mery. 

Hata hivyo Brigedia Jenerali (mstaafu), Mery Hiki amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumlinda mpaka kufika siku ya leo, pili  amewashukuru wazazi wake kwa kumzaa, kumtuza na kumpa msingi mzuri.

Hata hivyo amewashukuru Viongozi wa jeshi kwa kumuongoza kwani ametumikia jeshi kwa muda mwingi wa miaka 45.

"Nawashukuru viongozi wangu wa jeshi ukiangalia muda niliotuamika katika jeshi unaona kabisa niliingia nikiwa mtoto kwahiyo mimi nimelelewa zaidi na viongozi wa jeshi ninawashukuru sana sana." Amesema Brigedia Jenerali Mstaafu Mery.

Brigedia Jenerali Mstaafu Mery amewashukuru pia Umoja wa wanawake Tanzania kwani ndio waliosababisha kuanza kuandikisha wanawake jeshini.

Ukiangalia historia Jeshi, jeshi lilianza mwaka 1964 lakini mwanamke wa kwanza kuandikishwa jeshini ni 1972 ikiwa ni baada ya miaka nane .

Viongozi wale  walisimama na kudai kwamba jeshi nalo lichukue wanawake jeshini ndio maana na sisi tukachukuliwa. Amesema Brigedia Jenerali Mstaafu Mery.

Hata hivyo Brigedia Jenerali Mstaafu Mery amesema kuwa kwa wale wanaobaki wafuate nyayo za watangulizi wao ambao walifanya wakaendelea kuwepo jeshini.

Licha ya kuwa na cheo cha juu jeshini Brigedia Jenerali (mstaafu), Mery Hiki mpaka amestaafu alikuwa Mwambata jeshi nchini Burundi.

Kwa upande wake Luteni Jenerali (Mstaafu), Paul Masawo aliyetumikia jeshi kwa miaka  42 amesema kuwa jeshi siyo ajira.

"Jeshi si ajira, hakuna ajira huku ni unaandikishwa, fikira za kuingia jeshini kwaajiri ya ajira unaingia ujue unaweza ukafa au ukapona kwa sababu vita haina macho, kwahiyo suala la jeshi linahitaji uazalendo zaidi sio suala la kazi." Amesema Luteni Jenerali (Mstaafu), Masawo.

Amesema vijana ni vizuri wakaingia wale wenye sifa lakini kwa kufuata taratibu sahihi lakini wakijua wanaenda kuafanya kazi gani.

Hata hivyo amewaasa wananchi kuwa jeshi sio la mtu wala sio taasisi ya mtu mmoja we ananchi walipe ushirikiano jeshi hapa nchini. 

Ukiangalia changamoto za sasa kunavita zisizo rasmi ambayo adui humjui, ila ushirikiana na wananchi ili tusipoteze kitu kwani maendeleo yanakuja kwasababu kuna amani, hakuna amani hakuna maendeleo." Amesema Luteni Jenerali (Mstaafu), Masawo.

Luteni Jenerali (Mstaafu), Paul Masawo ambaye ametumikia jeshinkwa miaka 42 hadi anastaafu alikuwa Mkuu wa chuo cha ulinzi wa Taifa(NDC).

Nae Brigedia Jenerali mwenye cheo kikubwa kwa wanawake waliobaki jeshini na Kaimu wa tawi la manunuzi na ugavi jeshini, Hawa Kodi amesema kuwa anajivunia kuona waasisi wa wanawake wanajeshi wanakwendanao sawa.

"Tunatamani na sisi tunaobaki  kufikaa siku hii ya kustaafu kwa heshima. " Amesema Brigedia Jenerali Hawa.

Amesema kuwa misingi ya kukaa muda mrefu ni ile ile ambayo wengine wanapitia.

"Tunaahidi tunaobaki jeshini kuendeleza yale mazuri yote ambayo walikuwa wakiyafanya kwa mstakabalj wa taifa letu na jeshi letu kwa ujumla. Kwahiyo afande Hiki umestaafu leo kwa heshima na sisi tunaobaki tunatamani siku moja tufike kama mlivyofika nyie,  tutaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu kutekeleza maagizo kutoka ngazi za juu kama inavyoelekezwa." Amesema leo Brigedia Jenerali Hawa.
      

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2