Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SHIRIKISHO la Vyama vya Watu Wenye Ulamavu Tanzania(SHIVYAWATA) limesema linaipongeza Serikali kwa hatua mbalimbali ambazo imekuwa ikichukua dhidi ya kuweka mazingira mazuri kwa watu wenye ulemavu huku likitoa rai kwamba kuna umuhimu wa kuendelea kuimmbusha Serikali baadhi ya mambo muhimu ambayo yapo kwenye miongozo na sheria kuhusu walemavu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Shirikisho hilo kwa vyombo vya habari kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya kisheria na haki za watu wenye ulemavu Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Tungi Mwanjala amesema kimsingi kuna mambo mengi yamefanyika na wanaridhika nayo na ambayo hayajafanyiwa kazi wataendelea kuikumbusha Serikali.
"Tumefurahi kukutana na waandishi wa habari katika mafunzo haya ambayo yalijikita katika kuangalia sheria, miongozo na kanuni kuhusu watu wenye ulemavu, mlichojifunza kitakuwa daraja kati yetu na yenu ili muendelee kuandika habari zinazohusu watu wenye ulemavu.Ukweli tumepata muamko tutaendelea kushirkiana katika mambo tofauti tofauti.Karibuni kuandika habari za watu wenye ulemavu,"amesema Mwanjala.
Pia amesema kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ameviomba vyombo vya habari kuwa karibu na watu wenye ulemavu kwani kuna wawakilishi wao ambao wamepata afasi na kwamba tangu mwaka 1995 hadi sasa mwaka 20202 kumekuwepo na ongezeko la watu wenye ulemavu Bungeni ambako kwa Tanzania Bara wanazo nafasi tatu na Zanzibar nafasi mbili.
"Tulianza na mwakilishi mmoja lakini sasa wamefikia wawakilishi watatu kwa Tanzania Bara na watatu kwa Zanzibar na kweli ni kitu kizuri na tunaipongeza tunaipongeza Serikali yetu kwani imefanya jambo jema.Hata hivyo tunatamani tuwe na nafasi nyingi zaidi ya wawakilishi wa watu wenye ulemavu kwani shirikisho letu peke yale linavyama 10 na kila chama tunapenda kiwe na mwakilishi wake bungeni ili aseme yanayowahusu,"amesema.
Wakati huo huo amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu, wameshakutana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) na wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwani imejitahidi kwa asilimia kubwa kuangalia mambo yanayohusu watu wenye ulemavu na kuyapa kipaumbele.
"Kuna maeneo machache tu ndio hatuko sawa lakini tutaendelea kushirikiana na Serikali na tunaamini tutafika sehemu nzuri na kwa sababu naona kwa sehemu kubwa wanafanya kazi nzuri.Ujue watu wenye ulemavu na sisi ni watu kama walivyo watu wengine na wote tunaongozwa na hizo hizo sheria zilizopo nchini kwetu.
"Ni marekebisho madogo madogo tu yakifanyika tutakwenda sawa kwa mfano mikataba ya kimataifa inavyosema kuhusu watu wenye ulemavu, kuna baadhi ya vipengele Serikali imevisahau licha ya kuwepo katika sheria na mikataba, hivyo hatuna shaka Serikali hii itashiririkiana nasi kuendelea kuboresha kila ambacho tunadhani hakijafanyiwa kazi,"amesisitiza.
Ametoa mfano kuna mikataba inaeleza kuwa watu wenye ulemavu na wana haki ya kuchagua na kuchaguliwa na ukweli kwamba hayo ni sehemu ya mambo muhimu kwa jamii ya watu wenye ulemavu katika maisha yao ya kila siku.
"Tunawategemea sana waandishi wa habari, tuliyoliyozungumza katika mafunzo haya kila mtu ayafanyie kazi.Vyombo vya habari ni muhimili wa nne na ni muhimu kwetu kuendelea kutusaidia na kutusemea ili itusikie na kusaidiwa.Hivyo tunaomba ushirikiano wenu kadri mavyoona inafaa,"amesema Mwanjala.
Kwa upande wa wawashiriki katika mafunzo hayo wameeleza ambavyo mafunzo hayo yamewaongeza uelewa na ufahamu kuhusu sheria na haki za watu wenye ulemavu, hivyo wameahidi kuendelea kushirikiana nao.
Saum Bakari ambaye aliwakilisha Umoja wa Redio za Kijamii amesema huu si wakati wa walemavu kujiona wako nyuma na badala yake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kwa kuamini wanaweza na ukweli kuna viongozi wengi wenye ulemavu wameonesha uwezo mkubwa katika utumishi na wamekuwa chachua ya maendeleo ya nchi yetu.
Mwanasheria wa masuala ya watu wenye ulemavu Novath Rukwago akifafanua jambo wakati wa mafunzo maalum ya siku ya mbili yaliyoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania(SHIVYAWATA).Mafunzo hayo yalijikita zaidi kuzungumzia sheria na haki kwa watu wenye ulemavu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment