TWARIQA TANZANIA KUONGOZA WAISLAMU SHINYANGA KUOMBEA AMANI AGOSIT 29 | Tarimo Blog

 Msemaji wa Twariqa Tanzania Shekhe Haruna Hussein mwenye kanzu ya njano akiwa kwenye picha ya Pamoja na Viongozi wa wa Twariqa mkoa wa shinyanga.
 Picha ya Pamoja walipotembea na kuzungumza na wanafunzi wanaosoma dini ya Kiislamu mtaa wa majengo mkoani humo.
Msemaji wa Twariqa Tanzania Shekhe haruna Hussein akiwa na Darueshi Mussa kutoka nchini Uganda .

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WAISLAMU wametakiwa kuungana na kushirikiana katika kuwekeza  ndani ya jamii katika sekta Mbali Mbali, bila kujali Itikadi za kidini ili kuhakikisha kuwa dini ya Kiislamu inasonga mbele.

Hayo yameelezwa na Msemaji wa Taasisi Kongwe ya dini ya Kiislamu nchini ya Twariqa Shekhe Haruna Hussein, wakati akizungumza na wanachuo wa Chuo Cha Kiislamu kinachofahamika  Cha  Shekhe Aboubakari kilichopo Majengo Mapya mkoani Shinyanga.

Shekhe Haruna alisema kuwa katika kuwa ni vyema Waislamu wanatumia Neema Mbali Mbali vizuri ili kuhakikisha kuwa jamii inanufaika na dini lakini pia huduma Mbali mbali za kijamii kama shule,hospitali na nyinginezo.

"Tusiangalie Itikadi tulizonazo na msikae kinyonge Sana,tuipeleke dini mbele na ule mfumo wa Waislamu kusimama ufike mwisho Sasa,na viongozi wa Dini ya Kiislamu mguswe na matatizo ya Watanzania"alisema Shekhe Haruna.

Aidha aliwataka Viongozi wa Kiislamu kwenda Mbali Zaidi na kuacha kasumba ya kugombania Sadaka misikitini, badala yake wajenge zawia za kutosha ili kuhakikisha kuwa maadili hayapotei ndani ya jamii.

Nae Katibu Mkuu wa Twariqa Tanzania Yahya Athman Mkindi alisema kuwa ujio wa viongozi wakuu wa Twariqa Tanzania katika mkoa wa shinyanga ni maandalizi ya Kongamano kubwa la Amani linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya  Masjid Firdaus Ngokolo B,August 29.

Shekhe Mkindi alisema kuwa Kongamano hilo litaambatana na Harambee kwa ajili ya kiwanja Cha Zawiya na Markaz.

Katibu huyo alisema kuwa lengo la Kongamano hilo Ni kuombea Amani Taifa katika kuelekea Uchaguzi mkuu wa October 28, lakini pia kuwaasaa wagombea wa vyama vyote ambavyo vinashiriki uchaguzi kufanya kampeni za kistaarabu.

Kauli mbiu ya Kongamano hilo inasema kuwa "Uchaguzi Mkuu bila Vurugu Inawezekana".

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2