TCRA imeipiga fani ya sh.bilioni 11.89 kampuni ya Raha | Tarimo Blog

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi habari hatua walizozichukua kwa kampuni ya Raha Limited,Jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
 MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipiga Faini ya Sh.bilioni 11.89  Kampuni ya Raha Limited watoa huduma ya Internet  kwa makosa mbalimbali ikiwemo  kutumia masafa ya mawasiliano ya Radio katika wigo 1452-1482 MHZ bila kuwa na leseni halali kutoka TCRA tangu 24 Machi 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi James Kilaba amesema TCRA ilitoa leseni ya matumizi ya huduma za mawasiliano kimkoa, Leseni ya miundombinu ya  mawasiliano, Leseni   ya Kitaifa ya matumizi ya mawasiliano ya kieletroniki, leseni ya kufunga na kutengeneza vifaa vya Mawasiliano na Leseni ya matumizi ya namba kwa muda tofauti tofauti.

Mhandisi Kilaba amesema kampuni ya Raha baada ya kupata leseni walitakiwa kufanya mambo mbalimbali ikiwa kujenga,kusimika, kutunza ,kutumia na kusimamia miundombinu ya mikoa ya Dar es Salaam,Arusha na Tanga ifikapo Februari 2020 na Kilimanjaro ifikapo Septemba 2021 pamoja na kuandaa na kuwasiliasha mpango wa kuendeleza rasilimali Watu kwa Mamlaka hiyo.

Amesema kuwa katika kufanya kazi waliweza kuchukua masafa ya mawasiliano ya Radio mkoani Mtwara bila kubali na kupigwa faini sh.Bilioni 11.85.

Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Kilaba amesema kampuni Raha wanatakiwa kulipa faini sh.milioni 10 kwa kujenga Miundombinu ya mfumo wa mawasiliano kuendesha na kutoa huduma za mawasiliano mkoani Mtwara bila ya kuwa na Leseni kutoka TCRA, Kulipaa Faini ya Sh.milioni 5 kwa kutotimiza masharti ya Leseni baada ya kushindwa kutoa huduma mkoani Kagera Agasti 2019.

Aidha amesema kampuni hiyo inatakiwa kulipa sh.milioni 5 kushindwa  kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa mahesabu ya ndani ya miezi sita kuanzia mwaka wa hesabu na sh.milioni tano zingine ni kushindwa kuwasilisha mpango mkakati wa kuendeleza rasilimali Watu huku faini nyingi sh.milioni 10 kushindwa kutimiza  masharti ya leseni husani kushindwa kuomba upya kwa nuda uliopangwa.

"Masafa ni rasilimali ya Taifa haikopwi wala haiibwi na mtu yeyote."Amesema Kilaba.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2