Wateja wakipata huduma walipotembela Banda la RITA katika maonesho ya Nanenane.
Mtoa huduma wa RITA akizungumza na mteja katika maonesho ya nane nane.
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umewataka wananchi 1kuchangamkia huduma zinazotolewa na Wakala huyo kwa manufaa yao ya sasa na ya baadae.
Akizungumza na mwandishi katika viwanja vya nanenane mkoani Simiyu , Afisa habari Grace Kyasi amesema kuwa huduma za RITA ni huduma ambazo zinagusa maisha ya kila Mtanzania katika nyanja tofauti kama vile elimu, ajira, afya, mikopo ya elimu ya juu, ndoa, wosia na mirathi.
* Amesema "Jamii yetu inahitaji kufahamu kuwa huduma za RITA ni huduma ambazo haziepukiki kwa maana ya kugusa maisha yetu ya kila siku katika jamii yetu, kwa mfano, mtoto anapozaliwa atahitaji kupata cheti cha kuzaliwa, mtu anapofariki ndugu watahitaji kufuatilia cheti cha kifo cha marehemu, mtu anapofunga ndoa atatakiwa kusajili cheti chake cha ndoa vilevile tuna huduma ya kuandika na kuhifadhi wosia pamoja na usimamizi wa mirathi.
Huduma nyingine zitolewazo na RITA ni usajili wa talaka, usajili wa bodi za wadhamini pamoja na kuasili watoto. Amemalizia, Grace.
Hatahivyo hivi karibuni Wakala umeanzisha huduma ya usajili wa vizazi na vifo na uhakiki wa vyeti hivyo kwa njia ya mtandao ambapo mtu anaweza kuipata huduma hiyo popote alipo nchini.
Grace anasema kuwa "Katika kufikiria kusogeza huduma zetu karibu na wananchi, Wakala umeanzisha huduma ya usajili wa vizazi na vifo kwa njia ya mtandao popote ulipo, unaojulikana kama "E- Huduma" ambapo inapatikana katika tovuti ya Wakala ambayo ni https://bit.ly/3fkH0H9"Amesema.
RITA inawaasa wananchi kutumia huduma zake ili ziwafaidishe katika mahitaji yao mbalimbali na kuwakaribisha kutembelea banda lao namba 94 ambapo lipo karibu na banda la NIDA katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Wakala unatoa elimu kwa umma kuhusu huduma zake hizo ambapo katika ufunguzi wa maonesho hayo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais Serikali ya awamu ya tano, Samia Suluhu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment