WATAHINIWA 82,440 WAFAULU MTIHANI KIDATO CHA SITA, SHULE NANE ZA SERIKALI ZAINGIA 10 BORA | Tarimo Blog


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)Dkt.Charles Msonde 


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

BARAZA La Mitihani Tanzania (NECTA) leo Agosti 21, limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2020 huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 0.03 ukilinganisha na mwaka uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari leo visiwani Zanzibar Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Charles Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa 82,440 sawa na asilimia 98.35 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu wamefanya vizuri katika Mitihani wao.

Dkt. Msonde amesema kuwa kati ya watahiniwa hao waliofaulu wasichana ni 35,486 sawa na asilimia 99.07 na wavulana waliofaulu ni 46,954 ambao ni sawa na asilimia 97.81.

amesema kuwa watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 85,449 na waliofanya mtihani walikuwa 84,212 sawa na asilimia 98.49  na  watahiniwa 1,287 sawa na asilimia 1.51 hawakufanya Mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa na utoro.

Aidha amesema kuwa ufaulu kwa shule za Serikali umekua bora zaidi kuliko shule binafsi ambapo shule nane bora kati ya kumi ni shule za Serikali.

Shule nane za Serikali zilizoingia kwenye kumi bora ni pamoja na Kisimiri (Arusha) iliyoshika nafasi ya kwanza, Mzumbe (Morogoro,) Tabora girls (Tabora,) Tabora boys (Tabora,) Ilboro (Arusha,) Kibaha (Pwani,) Mwandet (Arusha) na Dareda iliyopo Mwanyara huku shule mbili binafsi zilizoingia kumi Bora ni Kemos (Bukoba) ambayo imeshika nafasi ya pili na Ahmes ya Pwani iliyoshika nafasi za tatu.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2