kwa niaba Serikali Gaguti ametoa pole hizo na salaam za Rambi Rambi kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Familia za Ndugu waliopatwa na maafa, ikiwa Ni pamoja na kupima Vinasaba Vya miili ya Marehemu, ikiwa pamoja na kugharamia shughuli zote za mazishi.
Aidha miongoni mwa Viongozi waliofika eneo Hilo ni pamoja na Mbunge Mteule Jumuiya ya Wanawake Tanzania Regina Zachwa ambae amekutana na Baadhi ya Wafiwa wakiwemo Viongozi wa Dini na Serikali na kutoa Pole na rambi rambi zake.
Kwa nyakati tofauti wamefika pia Afisa Elimu Mkoa Kagera, Mwenyekiti CCM Mkoa Kagera Bi. Costancia Buhiye, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkoa Kagera Wilbroad Mutabuzi pamoja na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Kamanda Saimon Sirro.
Kwa Upande wa Jeshi la Polisi, Kamanda Sirro amewaomba Wananchi kuwa wavumilivu na kutoa ushirikiano ili kubaini chanzo cha Moto huo, na kwamba ikiwa chanzo Cha ajali ikibainika kuwa ni kutokana na uzembe au miundo mbinu mbovu, hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Aidha Kamanda Sirro ameongeza kuwa Wamiliki wa Shule wanatakiwa kuwa na Kamati ya Usalama kuhakikisha Usalama wa Wanafunzi kuanzia majengo madhubuti na Imara, Ulinzi wa kutosha muda wote na kubaini wanafunzi watukutu ambao wengine hutumiwa katika matendo ya kiharifu.
Kufuatia Ajali hiyo na Msiba huo kitaifa, Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa CCM Taifa ameahirisha Mkutano wake wa Kampeini aliopanga kufanya Mkoani Kagera Manispaa ya Bukoba Septemba 15, na Sasa Mkutano huo utafanyika Tarehe 16 Septemba katika Viwanja vya Gymkhana.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment