DAWASA YAENDELEA KUTOA HUDUMA ONE STOP JAWABU NDANI YA VIWANJA VYA ZAKHIEM | Tarimo Blog



Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Temeke (Kulia) Alpha Ambokile akielezea jambo kwa Mgombea wa udiwani wa Kata ya Mbagala Kuu Shaban Abubakar (wa kwanza kushoto) alipotembelea banda la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwenye Kituo cha One Stop Jawabu yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ndani ya Viwanja vya Zakhiem Mbagala Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Afisa Mawasiliano Dawasa Joseph Mkonyi.

Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Temeke (Kulia) Alpha Ambokile akimkabidhi Mgombea wa udiwani wa Kata ya Mbagala Kuu Shaban Abubakar jarida la Uhuru alipotembelea banda la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwenye Kituo cha One Stop Jawabu yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ndani ya Viwanja vya Zakhiem Mbagala Jijini Dar es Salaam

Mgombea wa udiwani wa Kata ya Mbagala Kuu Shaban Abubakar (wa kwanza kushoto) akielezea changamoto ya maji ndani ya Kata ya Mbagala kuu kwa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Temeke (Kulia) Alpha Ambokile alipotembelea banda la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwenye Kituo cha One Stop Jawabu yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ndani ya Viwanja vya Zakhiem Mbagala Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Afisa Mawasiliano Dawasa Joseph Mkonyi.

Wananchi wakiendelea kupata huduma ndani ya Banda la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA ndani ya kituo cha One stop Jawabu kwenye Viwanja vya Zakhiem Mbagala Jijini Dar es Salaam

Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Temeke Alpha Ambokile akimsiliza moja kati ya wananchi waliojitokeza kutemebelea banda la Dawasa ndani ya Kituo cha One Stop Jawabu ndani ya Viwanja vya Zakhime Mbagala Jijini Dar es Salaam.


Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv 

WANANCHI  wa Wilaya ya Temeke wameombwa kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili uzàlishaji wa maji uendelee kuongezeka.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Temeke Alpha Ambokile katika Kituo cha One stop Jawabu Wilaya ya Temeke.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imekuwa ni moja ya taasisi za serikali zilizoshiriki maonesho ya One Stop Jawabu ndani ya Wilaya ya Temeke.

Maonesho hayo yamezinduliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dae es Salaam Abubakar Kunenge katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala yakihusisha taasisi mbalimbali za Kiserikali kwa pamoja kuja kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Wilaya ya Temeke.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Meneja wa Dawasa Mkoa wa Kihuduma Temeke Alpha Ambokile ameupongeza uongozi wa Manispaa ya Temeke kupitia kwa Mkuu wa Wilaya Godwin Gondwe kwa kuamua kuweka kituo ili wananchi wa Wilaya ya Temeke waweze kupata huduma.

Ambokile amesema, katika banda la Dawasa wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo maunganisho mapya kwa wateja wanaohitaji huduma za maji na kupokea malalamiko mbalimbali.

Ameeleza kuwa, wanaendelea kutatua kero ya maji ndani ya Mkoa wa Kihuduma Temeke na kuna mradi wa benki ya dunia wenye thamani ya Bilion 4 utakaoondla kero kwa maeneo ya Mbagala na Kijichi.

Akielezea ubadilishaji wa mabomba, Ambokile ameeleza kuwa kwa sasa mafundi wa Dawasa wanaendelea na kazi ya kubadilisha mtandao wa maji ambapo mabomba yake yana zaidi ya miaka 20 toka yawekwe.

Amefafanua kuwa, malalamiko ya ukosefu wa maji kwa maeneo baadhi ya Mbagala na Kijichi umekuwa ni mkubwa sana ila Dawasa imejipanga katika mwaka wa fedha kumaliza tatizo la maji ndani ya Mkoa wa kihuduma Dawasa Temeke.

Pia, ametawataka wananchi wa Temeke kuendelea kutunza chanzo cha maji cha mto Kizinga kwani ni moja ya chanzo kinachozalisha maji kwa muda mrefu na Dawasa wameweza kukitunza kwa kupanda miti aina ya mitomondo ambayo inatunza maji hata kipindi cha kiangazi mto haukauki.

Katika banda la Dawasa, liliweza pia kutembelewa na Mgombea wa Udiwani kata ya Mbagala Kuu Shaban Abubakar amewakata wananchi wa Kata ya Mbagala na Temeke kwa ujumla kujitokeza katika Viwanja vya Zakhiem kuja kutatua kero zao.

Amesema, One stop Jawabu isiishie kwa Wilaya ya Temeke tu bali iende zaidi hata wilaya zingine ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi zaidi.

" unajua hii One stop jawabu imekuja kutatua kero nyingi za wananchi, wengi walikuwa wanashindwa kwenda katika maofisi labda kutokana na muda au gharama za usafiri ila kuletwa huduma hii karibu wananchi wanaweza kumaliza na kutatua changamoto zao ndani ya eneo moja na muda mfupi,"amesema Abubakar.

Amewasihi wananchi wajitokeze kwa wingi katika Viwanja vya Zakhiem Mbagala ili kupata huduma zote kutoka katika taasisi mbalimbali za Kiserikali.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2