LEMA:80% MADIWANI WA CHADEMA HAWANA UWEZO WA KIFEDHA ,CHAMA KUTAFUTA FEDHA ILI KUWAWEZESHA KUFANYA KAMPENI | Tarimo Blog

Mgombea ubunge Jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni katika eneo la Olasiti mwisho wa Hiace kushoto kwake Ni mgombea udiwani wa kata hiyo ndugu Daniel Wangael Urioh.

======  ======  ======  ======

Na.Vero Ignatus

Mgombea ubunge Jimbo la Arusha  kwa tiketi ya Chama cha Demokasia na Maendeleo Chadema ndugu Godbless Lema Lema amesema kuwa  asilimia 80% ya madiwani wa chama hicho  hawana uwezo kifedha ila chama hicho kimejipanga kutafuta fedha zitakazowawezesha kufanya kampeni ambapo watahakikisha vijana wengi wanashika nafasi za uongozi kwani wanao uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kupigania haki na  maslahi ya wananchi kwa nguvu zao zote

''Lema:hakuna watu wanavunja moyo kama watanzania kwenye kazi ya siasa''alisema kazi hiyo ya ubunge kwake isingekuwa wito kutoka kwa Mungu angelikuwa ameshiacha tayari kwani tangia mwaka 2015 -2020 kila mwezi amekuwa akienda mahakamani mara 4, tangia ameanza kazi ya ubunge ameenda polisi mara 169 ambapo hajakata tamaa hadi leo japokuwa imefanyika bidii ya kuua chama hicho katika mkoa wa Ausha.

 Akimnadi mgombea wa udiwani kata ya Olasiti Daniel Wangael Urioh alisema kuwa kijana huyo ni mpambanaji hivyo aliwataka wakazi wa olasiti kutambua wajibu wao kwa kumchagua ili aweze kuwaletea maendeleo katika kata hiyo pamoja na ktatua changamoto zilizopo katika kata hiyo.

Kwa upande wake mgombea udiwani katika kata hiyo ya Olasiti ndygu Daniel Wangael Urioh alisema kuwa yeye ni mwalimu wa kwanza kwenye uchaguzi wa mwaka 2020  aliyeajirriwa serikalini,kuthubutu kugombea kupitia chama cha upinzani ,ambapo alijitambulisha kama kijana jasiri ,mwenye maono na mwenye dhamira ya dhati ya kulitumikia taifa lake 

Amesema kuwa ameanza kuonyesha kwa kugombea nafasi ya udiwani huku akiwa na ndoto kubwa ya kufanya vyema katika ngazi za juu zaidi kwaajili ya wananchi na Taifa kwa ujumla na kuhakikisha kuwa kunakuwa na uongozi bora,shirikishi na wenye utu.

Aidha ameahidi kuwa atakapopatiwa nafasi hiyo ataitumia vyema katika kupambania huduma za kijamii ikiwemo Afya,maji,miundombinu ,stendi na kuwa na kituo cha polisi kwaajili ya usalama wa wananchi katika kata hiyo ya Olasiti.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2