WILAYA Kisarawe yavutia kwa wawekezaji mbalimbali kutokana na miundomini ambayo serikali ya awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli imetekeleza.
Hayo yamesemwa na Mwanadiplomasia, Raphael Maganga katika uzinduzi wa kampeni ya CCM, Jimbo la Kisarawe akimnadi Mgombea wa jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri ofisi ya Raisi Tamisemi, Suleiman Jafo.
“Jimbo la Kisarawe, limekuwa kivutio kikubwa sana kwa wawekezaji kwasababu ya miundomini ambayo serikali ya awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli imetekeleza.” Amesema Maganga
Akimshukuru Waziri Jafo, Maganga aliongezea “ Nimefurahishwa sana kuona mmetenga eneo, Kata ya Kazimzubwi Eneo la Visegese limepimwa Ekari 500s Eneo kwaajili ya viwanda ni Ekari 1100 Makaazii ni 1800 na Viwanja vilivyo tayari ni 291 kuwa eneo la viwanda, Jafo, upendo ulionao kwawana Kisarawe ni mkubwa sana, maana Umeme mmewaletea, maji mmewaletea, barabara ya The Great Nyerere Road mnaijenga kwa hadhi ya Lami kwenda Mbuga ya wanyama ya Nyerere."Amesema Maganga
Hata hivyo maganga amesema kuwa wafanyabiashara watafurika Kisarawe kuwekeza kwenye viwanda, hivyo basi Wanakisarawe watapata ajira kutokana na uwekezaji huu.
Licha ya hilo alilisisitiza kuwa wafanyabiashara wachangamkie fursa hizo katika jimbo la kisarawe maana miundombinu yote muhimu tayari ishawekwa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment