Mratibu wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Paradigm Initiative Afrika, Peter Mmbando akizungumza na waandishi wa habari na mashirika yasiyo ya Kiserikali katika mkutano wa kujadili masuala ya habari katika mitandao ya jamii na internet ,jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria wa Shirika la Organsation for Peace and Consensus Building (OPCB) Ice Erick akichangia mada katika mkutano namna ya kufuata sheria katika uhabarishaji wa habari,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Serengeti Bytes Kennedy Mmari akichangia mada katika mkutano namna ya kufuata sheria za katika kuhabarisha jamii katika masuala ya Mitandao
Baadhi ya wadau wakifatilia mada kwa njia ya mtandao
Picha ya pamoja ya waandishi habari na mashirika yasiyo ya kiserikali mara baada ya kumaliizika mkutano kwa njia ya mtandao.
*Matumizi ya Mitandao ya Jamii, Internet yatakiwa kuwa salama katika upatikanaji wa habari
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kufuata taratibu za uandishi wa habari zilizowekwa ili kulinda haki za wananchi kupata taarifa hasa katika matumizi ya mitandao ya jamii pamoja na Internet .
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliokutanisha wadau kuangalia na kujadiliana namna ya sheria ya mtandao kwa Tanzania jijini Dar es Salaam Mratibu wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Paradigm Initiative Afrika, Peter Mmbando amesema kuwa uhuru wa vyombo vya habari na sheria katika matumizi ya mitandao na internet ni kuangalia namna ya kusaidia kuboresha ufanisi, bora ya upashanaji wa habari na kufuata taratibu zilizowekwa katika kupasha habari jamii zenye kuzingatia ukweli na uhakika.
“Rai kwa Wanahabari kufuata taratibu ambazo zimewekwa na mamlaka husika ili kulinda haki za wananchi katika kuwapasha habari,Habari zinatakiwa ziwe za kweli hazitakiwi ziwe za kutengeneza kwani mtu anapodanganya jamii kwa sauti/video anaharibu taratibu uliowekwa kisheria.”Amesema.
Aidha aliyaonya makundi ambayo hayajasomea mambo ya habari, wanatakiwa kuacha kutoa taarifa ambazo hazina ukweli na kupotosha umma ni kuharibu utaratibu za mamlaka.
Kwa upande wake Ice Erick kutoka shirika masuala ya umoja, Amani na maendeleo(OPCB), alisema kupitia mkutano huo wamejifunz amambo mengi yanayo husu matumizi sahihi ya mitandao na kuongeza kuwa changamoto za matumizi ya kimtandao ni jukumu lao kuhakikisha watu ambao wanaweza kupata maafa kutokana na matumizi yasiyosahihi.
“Nadhani katika matumizi ya mtandao ni kuna umhimu wa kuchukua hatua nzuri kwa sasa kuiga mfano kwa nchi zingine kama jambo litakuwa na matokeo mazuri kutoka nchi zingine kuweza kulinda uhuru wa matumizi ya mtandao.”Amesema.
Hata hivyo mmoja wa mshiriki wa mkutano huo, Kenedy Mmari alisema majadiliano hayo muhimu hasa katika kushirikisha wadau katika michakato mbalimbali ya uundaji wa sera na sharia inayosimamia sekta mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya kimtandao na vyombo vya habari.
“Katika miaka ya hivi karibuni sheria nyingi zenye mlengo mzuri zinazingatia habari sahihi mtandaoni, usimamizi mzuri wa mtandaoni lakini sababau za msingi kunapokuwa hakuna msimamizi wa habari za ukweli inaleta athari.”Alisema.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment