MGOMBEA UBUNGE CHEDEMA AAHIDI KUPELEKA MAENDELEO SINGIDA | Tarimo Blog



Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Rehema James Mkoha (katikati) akiwasili  jana Uwanja wa Bombadia zamani Peoples kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa kufungua kampeni ya uchaguzi ngazi ya mkoa. 
Wafuasi wa chama hicho na wananchi wakiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu, akihutubia.
Wafuasi wa chama hicho na wananchi wakiwa katika mkutano huo.

Askari polisi wakiimarisha ulinzi kwenye mkutano huo.


Mkutano ukiendelea.


Mwenyekiti wa Wilaya ya Singida Mjini wa Chadema, Mutta Anselimi Adrian, akizungumza kwenye mkutano huo.


Kijana akionesha umahiri wa kucheza sarakasi kwenye mkutano huo.

Wafuasi wa chama hicho na wananchi wakiwa katika mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya  Singida Mjini, Gideon Murya, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida, Emmanuel Jingu, akizungumza kwenye mkutano huo.

Wagombea nafasi ya udiwani wakitambulishwa.


Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Mashariki, Noeli Hema, akizungumza.


Mkutano ukiendelea.


Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Mkoa wa Singida, Emmanuel Lissu, akizungumza.


Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (CHADEMA), Josephine Lemoyan, akizungumza kwenye mkutano huo na kuomba kura zote wapigiwe wagombea wa Chadema.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Rehema James Mkoha (wa pili kulia), akiserebuka na wakina mama kwenye mkutano huo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkalama kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Oscar Kapalale, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Taifa, Mwalimu John Pambalu, akizungumza kwenye mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.


Viongozi wakiwa Jukwaa Kuu.


Utambulisho madiwani.

Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu, (wa pili kushoto) akiwanadi wagombea ubunge wakiwemo na wa Viti Maalumu.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Rehema James Mkoha, akihutubia mamia ya wananchi na wafuasi wa chama hicho wakati wa ufunguzi rasmi wa kampeni za chama hicho ngazi ya mkoa.
Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu, akizungumza na wananchi na wafuasi wa chama hicho baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Na Mwandishi Wetu, Singida
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Rehema James Mkoha amesema ameamua kugombea nafasi hiyo ili awe mdau wa maendeleo ndani ya jimbo hilo pamoja  Singida nzima.

Mkoha ameyasema hayo wakati akihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kufungua kampeni ya uchaguzi ngazi ya mkoa uliofanyika Uwanja wa Bombadia zamani Peoples uliopo mjini hapa.

"Nafasi hii ya ubunge sijaanza kugombea leo nina miaka 10 sasa nataka kuwa mdau wa maendeleo katika jimbo ili la Singida mjini kwa masilahi ya wanasingida na sio kama wanavyojifananisha  baadhi ya viongozi na nzi aliyetumbukia kwenye maziwa ambaye hafi kutokana na kuyanyonya akimaanisha baada ya kupata madaraka." alisema Mkoha.

Akifafanua kauli hiyo amesema Mbunge yeyote makini anatakiwa kabla hajaenda bungeni kwanza ajue kero za wananchi wake kuanzia ngazi ya mashina, kata mpaka halmashauri na kurudisha mrejesho kwa walengwa ambao ni wananchi kile alicho washilikisha bungeni na majibu yake.

Amesema Mbunge wa Jimbo la Singida mjini kwa lugha nyingine ni diwani wa kata 18 ambazo anaahidi atahakikisha kila wazo la maendeleo na kero zilizopo kwenye kata hizo anaziwasilisha kwenye mamlaka husika kwa maana ya bunge kwa wakati na si kama alivyokuwa akifanya mbunge aliyekuwapo ambaye anagombea tena nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha Mkoha akizungumzia fedha za mfuko wa jimbo amesema atahakikisha kwenye kila milioni 40 itakayotolewa kwa miezi mitatu inakwenda kugawanywa katika kutatua kero zote za msingi kwenye jimbo hilo.

Katika hatua nyingine Mkoha ameahidi kuwaunganisha wanawake wote wa jimbo hilo ili wawe na nguvu ya pamoja ya kiuchumi kwa lengo la kuleta ustawi kwa maendeleo ya wana Singida.

Akizungumza kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu amesema siasa ya zamani ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere haipo sawa na ya sasa kwani ya wakati wake ilikuwa imejaa upendo na mshikamano miongoni mwa jamii tofauti na ya sasa.

Mkutano huo ulikwenda sambamba na kuwatambulisha wagombea wa nafasi ya ubunge na udiwani wa mkoa mzima.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2