Na Said Mwishehe,Michuzi Tv-Sengerema
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwamba katika kipindi cha miaka mitano ijayo ya uongozi iwapo watamchagua kuongoza tena nchi kwa miaka mitano atahakikisha anaendelea kuboresha huduma za miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami.
Pia amesema kwa sasa wameanza ujenzi wa daraja la Busisi katika Ziwa Victoria lenye urefu wa kilometa 3.2 na jumla ya Sh.bilioni 700 zitatumika katika ujenzi huo na baada ya kukamilika Sengerema itakuwa kama Ulaya.
Dk.Magufuli amesema hayo leo Septemba 8,2020 alipokuwa akizungumza na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Sengerema ambapo amesisitiza kuwa kupitia Ilani ya Uchaguzi Mkuu kuna mambo makubwa yanakwenda kufanya kwa ajili ya maendeleo ya wananchi hao.
Akiwa katika eneo la kivuko hicho cha Busisi, Dk.Magufuli amefafanua kuwa daraja hilo litakamilika kwa kipindi kilichopangwa kwani fedha zipo na zote zimetolewa na Serikali na kwamba kukamilika kwa daraja hilo kitakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya wananchi.
“Daraja hili ni muhimu kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi, hivyo litachochea ukuaji uchumi, lakini ndugu zangu hata wale ambao watakuwa wanataka kufunga watakuja hapa katika daraja maana kutakuwa kama Ulaya,”amesema Dk.Magufuli na kuwaomba wananchi kuchagua Rais,wabunge na madiwani wa CCM ili kuendelea na mipango mizuri ya kupeleka maendeleo kwa wananchi.
Wakati huo huo Dk.Magufuli akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Sengerema Mjini , amewakumbusha wananchi hao kuwa yeye hapo ni nyumbani kwani alipoanza kufanya kazi yake alianzia Sengerema kwa kufundisha Shule ya Sekonfari Sengerema.
“Kwa hiyo mimi ni mwenyeji, maeneo yote nayafahamu, Sengerema haikuwa hivi katika miaka ya nyuma.Nyakamilo ndio ilikuwa shida zaidi, kuliwa na changamoto mkubwa wa barabara na kulikuwa na basi moja ambalo lilikuwa linafanya safari kwa wiki mara mbili tu.
“Maisha ya Sengerema nayafahamu hospitali ilikuwa ya Misheni ambayo ilikuwa ikitoa huduma za afya, na ukiikosa hapo inabidi ukatafute Geita au Mwanza.Miaka mitano iliyopita wananchi wa Sengerema mliamua kuichagua CCM.
“Nawashukuru sana, yapo mambo mengi tuliahidi, kuna mabadiliko makubwa sana yamefanyika hapa Sengerema, maendeleo ni makubwa na hata ujenzi wa nyumba za kisasa unaendelea kwa kasi, mji unazidi kukua, “amesema Dk.Magufuli huku akiwahakikishia wananchi hayo yote ambayo yametolewa kama ombi kwa ajili ya maendeleo yao yatatekelezwa.
Kuhusu maji, amesema katika kipindi cha miaka mitano jumla ya Sh.bilioni 27.2 zimetumika kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya maji ukiwemo mradi mkubwa wa maji wa Sengerema –Nyamagazo uligharimu Sh.bilioni 22 na miradi mingine inaendelea.
“Ndio maana tumekuja kuomba kura ili miradi yote iweze kukamilika, tumetenga fedha zote hizo ili kukamilisha miradi ya maji,”amesema.
Kuhusu elimu amesema katika kipindi cha miaka mitano , Serikali imefanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo ukarabati wa shule kongwe, ujenzi wa miundombinu ya shule maalum ya Sengerema.Pia wameendelea kutao elimu bure kwa miaka mitano.
Akizungumzia sekta ya afya,Dk.Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano Sengerema kumejengwa hospitali mbili za Sengerema na Buchosa, ujenzi wa vituo vya afya na zahanati na lengo ni lengo ni kuhakikisha afya za Watanzania zinaimarika.
”Ili Mtanzania aweze kufanya kazi anahitaji kuwa na afya nyema ,tumeboresha upatikani wa dawa, bajeti imeongezeka kutoka Sh.bilioni 31 hadi Sh.bilioni 270, tumefanya haya ili afya za watanzania ziweze kuimarika na ndio maana Ilani ya Uchaguzi Mkuu imeeleza kwa kina yanayokwenda kufanyika kwa maendeleo ya wananchi,”amesema.
Amefafanua kuwa Serikali ilianza na kuimarisha huduma za afya na baadae utakuja mpango wa bima ya afya kwa Watanzania.
”Tumewabana mafisadi na kudhibiti upotevu wa fedha za umma na fedha ambazo zinapatikana zinakwenda kuleta maendeleo ya Watanzania wote yakiwemo ya wananchi wa Sengerema,”amesema.
Kwa upande wa barabara amesema anafahamu kuna ombi la barabara ya kutoka Sengerema ,Nyamazugo mpaka Nyehunge yenye urefu wa kilometa 54.67 ambayo amesema ataitolea maelekezo baada ya kuikagua.
Dk.Magufuli amesema ili kupatikana kwa maendeleo hayo kwa wananchi wa Sengerema wanatakiwa kuchagua Rais , wabunge na madiwani wa CCM.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment