Bi Grace Faustin (46) mkazi wa kijiji cha Diling'ang akinyoosha mkono kama ishara kuonyesha ukubwa wa eneo lake alilopimiwa na kupata hati za kimila ambapo aliweza kupatiwa hekta mbili.
Bi Eser Gitamani anasema mumewe alimuacha na kuoa mke mwingine,mwanzoni tulikuwa haturuhusiwi kabisa kumiliki ardhi sisi wanawake wa jamii ya kifugaji hivi sasa namiliki heka mbili baada ya kupatiwa hati ya Kimila
Wakinamama kutoka kijiji cha Diling'ang wilaya ya Hanan'g mkoa wa manyara wakiangalia ramani ya Kijiji chai baada ya kuhakikiwa mipaka.
Baadhi ya wakinamama kutoka kijiji cha Diling'ang wilaya ya Hanang' mkoa wa Manyara wakiwa na hati za kimila mara baada ya kupimiwa maeneo yao ambapo hivi sasa na wao wana haki ya kumiliki ardhi
Bi Grace Faustin akiwa na mama take mzazi wakiwa wamebakia vazi la asili mara baada ya wageni kutembelea nyumbani kwao na kuona eneo la shamba analomiliki baada ya kupatiwa hati miliki ya Kimila,anasema Vazi hilo huvaliwa kwa shughuli maalum na ni la heshima kubwa kutokana na Mila na desturi ya kabila lao.
Albert Masuja Afisa progam Msaidizi wa UCRT akiwa na Bi.Garace Faustin aliyevalia vazi ka asili la jamii ya Kibarbaig
Mwenyekiti wa Kijiji mwenyekiti wa kijiji cha Diling'ang Michael Safari anasema walipokea mradi huo kutoka UCRT pamoja na Oxfam kwaajili ya usaidizi wa kupima ardhi na kupatiwa hati za kimila kwa wanawake 100
Grace Faustin mkazi wa kijiji cha Giling'ang akionyesha hati miliki yake ya Kimila baada ya kupimiwa Ardhi ambayo anamiliki kwa Sasa.
Bi Eser Gitamani akionyesha eneo lake lenye ukubwa wa hekari mbili anazozimiliki sasa baada ya kupatiwa hati tofauti na ilivyokuwa awali alikuwa haruhusiwi
Na.Vero Ignatus,Manyara
Takribani 80% ya wananchi wa vijijini hutegemea ardhi kwa maisha yao ya kila siku kwa chakula,kipato na mahitaji mengine,kwani ardhi ni rasilimali adimu ambayo hushindaniwa na watu au shughuli mbalimbali, hivyo kufanya iwe na thamani kubwa,ambapo humilikiwa Kiserikali, Kimila kwa sheria,kanuni na taratibu zinazokubalika.
Baadhi ya mila na desruri nyingi katika jamii haswa za kifugaji zinawanyanyasa wanawake ambao wamezidi kuonyesha uwezo, mkubwa na utashi wa maendeleo, ambapo wanakosa uwezeshaji,jambo ambalo jamii inatakiwa kupinga mila desturi ambazo ni kandamizi kwa wanawake pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Diling'ang Michael Safari anasema walipokea mradi wa Gift kutoka Oxfam-UCRT , wakaalika Serikali ya kijiji,ndipo wakaitisha mkutano mkuu wa kijiji na wakatoa semina kwa wananchi juu ya umuhimu wa kumiliki ardhi haswa kwa wanawake pamoja na upimaji wa ardhi
Michael anasema Oxfam iliweza kuwapatiwa elimu kutambua faida za upimaji wa ardhi kama ,kuondoa tatizo la migogoro ya mipaka ya marakwa mara,urasimishaji,kupanga matumizi ya ardhi ili kuchangia katika wilaya yao ,kuongeza thamani ya viwanja na eneo lililopimwa,kupata mikopo mbalimbali kwa kupitia rasilimali ya ardhi,utambulisho wa kiwanja kilipo.
Anasema kijiji cha Diling'ang kiliweza kuwaalika vijiji vya jirani ambavyo ni Bassutu,Endamudayga,Gidika kwaajili ya kuhakiki mipaka,ambapo baada ya zoezi hilo kukamilika Oxfam wakasema ni vyema kuingia katika miradi yote ya iliyopo kijijini hapo zikiwemo nyumba za ibada ,eneo la malisho ,ofisi ya kijiji ,shule,minada na shamba la chama vyote vilihakikiwa mipaka yake
Michael anasema UCRT walitoa fursa kwaajili ya kuwapimia ardhi wakinamama ,walemavu,wazee,wasio na uwezo,,wajane,kwa ujumla wale waliokuwa hawana uwezo ndani ya kijiji hicho ambao wamefutiwa michango yao, waliweza kupimiwa wanawake 100 ambwanamiliki ardhi iliyopimwa,aidha mradi huo ulikuwa wa miezi 6 ambapo sasa umefika kikomo na waliweza kufikia kaya 391
Afisa programu kutoka UCRT Albert Masuja: nia kuu ya mradi huo ni kushughulikia suala la haki za wanawake na usawa katika jamii ambazo kwa mila na desturi za jamii ya kibarbaigi wanawake hawana haki ya kumiliki ardhi,mali isipokuwa kwa kudhaminiwa na watoto wao,ilihali watoto hao wakikua udhamini unakoma,jambo hilo lilieta madhara makubwa kwa wanawake kwani waliwekwa pembezoni,walionewa walifanyiwa ukatili na hawakushirikishwa katika uchumi na walidumaa kimaendeleo
Masuja:Awali ardhi ilikuwa inauzwa sana na wanaume, baba anakwenda kilabuni anarudi anasema kuanzia leo nimeamua kumkodishia fulani bila ridhaa ya familia,wazee wa boma wanafanya maamuzi wao kama wao bila kuishirikisha familia na kwao waliona jambo la kawaida sana maana mwanamke hana thamani.
''Hivyo sisi tumeona katika jamii ya kifugaji jamii ya Kibarbaig wimbi kubwa sana ya ardhi ikiondoka kwa kusababushwa na wanaume wazee ,wababa wa familia,tukaona kwamba ili tupunguze mianya hiyo lazima wanawake wapewe kipaumbele cha kumiliki shamba kwanza ni waaminifu,wanalinsa familia hata ikitokea dhoruba gani mwanamke hawezi kuacha familia'' anasema Masuja
Masuja anasema kuwa wao waliona kuwa wakiwamilikisha wanawake ardhi wanaitetea sehemu kubwa ya jamii na ardhi ikabakia salama lakini hawakuishia hapo waliona kuwa ardhi ya umma ikilindwa na wenyewe ni nguvu zaidi,mf.eneo la malisho haliwezi kuvamiwa na mtu yeyeote kwasababu linalindwa na chama cha wafugaji wakitumia hati yao amabayo ipo kisheria.
Mwanzo tuliitwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji nakujulishwa kuwa kuna msaada unaokuja wa Oxfam,tukapewa semina wanawake wasiojiweza kiuchumi,baada ya mafunzo tukaambiwa tutapimiwa ardhi na tukaitikia wito huo,basi tukapimiwa ardhi na fasi yangu ikafurahi sana kuwa mmoja wawanawake waliopimiwa ardhi na nimepata hati miliki bila msukosuko wowote''Anasema Grace Faustin (46) mama wawatoto 4 mkazi wa kijiji cha Diling'ang''
Anaendelea: kwamba eneo analoishi kwa sasa ni la wazazi,na mumewe alikuwa anaishi kwa ndugu zake baada ya hapo hakuelewana na familia yake ikabidi aje aishi kwa nyumbani kwa baba mkwe wake mwanamke(wazazi wa mkewe)baada ya muda akabadilika na alikuwa na mifugo michache akataka ahame aende porini ,anasema yeye Grace alikakataa kwani baada ya muda baba alifariki,na mama ni mzee hana usaidizi na yeye kwa mama ndiye mtoto pekee.
Hivyo baada ya kubishana kwa muda mrefu bila ya kuwa na muafaka ,mume wake aliamua kuondoka na mifugo yake akakaa huko kwa mika 3,baadae akarudi anasema kuwa siyo mpenda maendeleo wala hapendi watoto wasome, ila alipambana akapata msaada na akamshirikisha mume kwamba mtoto amefaulu wampeleke shule akanijibu hahitaji kusikia hizo habari,basi akapambana mtoto akafaulu na antarajia kuingi chuo kikuu sasa.
''Kikwetu mzee ndiyo anayeweza kumiliki vitu vyote ,anaweza akaja na kusema mimi nitauza shamba, bahati nzuri kwasababu mama yupo atakuwa hana uwezo sana ,lakini ikitokea bahati mbaya mama akafariki atakuwa na amri juu ya eneo, ila ninafuraha kubwa kwasababu hati hii kwangu inanipa ulinzi zaidi na hakuna mtu yeyote anayeweza kuninyang'anya kwani natambulika kisheria''.
Kwa upande wake bi Ester kutoka kijiji cha Diling'ang anasema kuwa yeye alikuwa anaishi na mumewe kwa muda mrefu wakashindwana na wameachana kisheria,hivyo alivyosikia kuna upimaji wa ardhi bure ndiyo ikawa sababu ya mimi kupenda nami nipimiwe ardhi,anasema hati hiyo aliyoipata itamsaidia kwasababu baadae kwake itakuwa ushaidi wa kutosha.
''Tulipokuwa tunaishi mimi nayeye akiamka na kisirani anakuja ananipiga anavyotaka au ananifukuza ananiambia toka nenda kwenu basi na mimi naondoka naenda kwa ndugu na ninaendelea kuteseka ninapoenda,sasahivi nashukuru kwasababu mambo kama haya atakuwa anaogopa kwasababu namiliki kihalali''.Anasema Ester mama wa watoto wawili
Anasema japokuwa ameachwa kwa talaka kisheria ila wakati wa upimaji ardhi mumewe huyo alikubali kuwa (mtalaka wake) apimiwe takribani hekari mbili katika sehemu shamba,
Aidha hati miliki kimila ina hadhi sawa ambavyo kwa hali yeyote sawa na hati miliki inayotolewa kisheria,yaweza kutolewa na halmashauri ya kijiji kwa raia,familia,kikundi cha raia wawili au zaidi au chombo chochote chenye hadhi ya shirika ambacho wabia wake wengi ni raia,yaweza kutolewa kwenye ardhi ya kijiji au ardhi hifadhi,yaweza kumilikiwa kwa muda usio na mkomo ,inasimamiwa na sheria za kimila kuhusiana na masuala yeyeote miongoni mwa watu ndani ya kijiji chenyewe,kwa kuzingatia malipo na ada ya kodi au kwa shirika au mtu mmoja mwenye eneo la makazi eneo lakijiji
Cheti cha haki miliki ya Kimila hutolewa kwa fomu iliyoainishwa na kutiwa saini,kuwekewa lakiri na kusajiliwa na Afisa ardhi wilaya ambapo kijiji kipo,cheti hicho kittiwa saini na kuwekwa alama na mtu ambaye atapewa haki miliki ya kimila,kitatiwa saini na mwenyekiti pamoja na katibu wa halmashauri ya kijiji.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment