………………………………………………….
Tume ya Taifa ya Uchagzui katika kikao chake cha jana tarehe 9 Septemba, 2020 imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa 67. Kati ya hizo, rufaa 22 ni za Wagombea Ubunge na 45 ni za Wagombea Udiwani.
Maamuzi ya rufaa za wagombea Ubunge ni kama ifuatavyo:-
i. Imekubali rufaa 19 na kuwarejesha wagombea husika katika orodha ya wagombea. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Majimbo ya Tunduru Kaskazini, Mbeya Vijijini, Songea Mjini, Karagwe, Ulanga, Chemba, Tanga, Kibamba, Nyasa, Same Mashariki, Buhigwe, Mufindi Kusini, Muheza, Tabora Kaskazini, Ubungo (2) na Kigamboni (3).
ii. Imekataa rufaa 3 za kupinga walioteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Majimbo ya Kalambo, Kigamboni na Muheza.
Aidha, Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 45 za Madiwani, kama ifuatavyo;-
i. Imekubali rufaa 26 na kuwarejesha wagombea husika katika orodha ya wagombea Udiwani. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Kingolwira (Morogoro Mjini), Kilakala (Morogoro Mjini), Bwera (Chato), Bugene (Karagwe Mjini), Babati (Babati Mjini), Mzingani (Tanga), Bukindo (Ukerewe), Kihanga (Karagwe), Central (Tanga Mjini), Muriti (Ukerewe), Namagondo (Ukerewe), Kakukuru (Ukerewe), Bukindo (Ukerewe), Mindu (Morogoro Mjini), Kitangiri (Ilemela), Ilemela (Ilemela), Buzuruga (Ilemela), Magaoni (Tanga), Uwanja wa Taifa (Morogoro Mjini), Kerege (Bagamoyo), Chemchem (Kondoa Mjini), Tungi (Morogoro Mjini), Ndama (Karagwe), Mbuyuni (Morogoro Mjini), Kiwanja cha Ndege (Morogoro Mjini), Igurwa (Karagwe Mjini)
ii. Imekataa rufaa 16 za wagombea ambao hawakuteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Ilangala (Ukerewe), Kandawe (Magu), Mazimbu (Morogoro Mjini), Msindo (Same Magharibi), Kiomoni (Tanga Mjini), Magaoni (Tanga Mjini), Usagara (Tanga Mjini), Kayanga (Ukerewe), Namilembe (Ukerewe), Nakatunguru (Ukerewe), Bwiro (Ukerewe), Kihanga (Karagwe), Kisegese (Mkuranga), Mnyajani (Tanga Mjini) na Rufaa mbili kutoka Kata ya Ngoma (Ukerewe).
iii. Imekataa rufaa 3 za kupinga walioteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata ya Ipwani (Mbarali), Ilemela (Ilemela) na Kichangani (Ulanga).
Idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea Ubunge zilizofanyiwa uamuzi na Tume hadi sasa kufikia 111 na za wagombea Udiwani 45. Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo. Wahusika wa rufaa hizo wameanza kujulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment