NA MWANDISHI WETU, MASASI.
MGOMBEA Ubunge wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Masasi Mjini, lililopo Mkoani Mtwara, Geoffrey Mwambe amewaomba wananchi wa Jimbo hilo kumpa ridhaa ya kuwa Mbunge wao ili aweze kuwaletea maendeleo.
Mwambe alisema hayo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Napupa jana ambapo alisema kuwa, Jimbo hilo lina changamoto mbalimbali ikiwamo miundombinu mibovu ya barabara, umeme na maji katika baadhi ya maeneo.
Alisema kuwa, ikiwa wananchi watamchagua kuongoza jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu, atashirikiana na Serikali ili kuhakikisha wanatatua changamoto hizo.
Mwambe aliongeza kuwa, Wananchi hao pia wanajishushulisha na mazao ya kilimo cha ufuta, korosho, choroko na mbaazi, hivyo basi atahakikisha wananchi wanapata masoko ya uhakika ya kuuza bidhaa zao ili waweze kupata fedha ambazo zitawakwamua kiuchumi.
"Ikiwa mtanichagua Oktoba mwaka huu, nitahakikisha nashirikiana na Serikali ili kutafuta masoko ya mazao yao pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara ili wakulima wapate urahisi wa kusafirisha mazao yao kutoka shambani."alisema Geoffrey Mwambe.
Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, maisha ya wananchi yatabadirika na kupiga hatua za kimaendeleo.
Kwa upande wa changamoto za umeme, maji na huduma za afya ndani ya Jimbo hilo, ameahidi atahakikisha anatatua changamoto hizo hatua kwa hatua ili wananchi waweze kupata huduma hizo pahala walipo.
"Nimejipanga kuhakikisha wananchi wa Masasi Mjini wanapata maendeleo.
Nitashirikiana na Serikali kila nyanja ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na kunufaika na rasilimali zao." alisema Geoffrey Mwambe.
Aliongeza kuwa, amejipanga kuhakikisha anafanya kampeni za kistaarabu ambazo zitasaidia wananchi kumuamini na kumchagua kwenye uchaguzi mkuu hiyo Oktoba 28.
Aidha, pia Mwambe mbali ya kujiombea kura, pia aliweza kumuombea kura nyingi na za kishindi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Madiwani wote ndani ya jimbo hilo la Masasi Mjini.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment