Polisi wa Belarusi wazuia waandamanaji 250 huko Minsk | Tarimo Blog

Na Lusajo Frank, Michuzi tv 
POLISI wa Belarusi wawashikilia kwa nguvu mamia ya waandamanaji huku makumi ya maelfu wakizidi kuongezeka katika mji mkuu Minsk kabla ya kufanyika mazungumzo kati ya Rais wa Belarus Alexander Lukashenko na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Polisi walioficha uso wakiwa wamevalia sare na nguo za wazi walimkamata watu waliokusanyika kwa maandamano ya "March of Heroes" siku ya Jumapili, wakiwasukuma au kuwapiga ngumi, video iliyochapishwa kwenye wavuti ya habari ya Belarusi Tut.by ilionyesha.

"Askari walizunguka mwandamanaji na kuwapiga alisema mmoja wa waandamanaji ambaye hakujulikana aliliambia shirika la habari la Reuters.

Alexander Lukashenko amekuwa madarakani kwa takribani miaka 26 anakabiliwa na hasira ya umma baada ya kutangaza ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 9 mwaka huu, ambapo wapinzani wake walisema ulikuwa wizi. 

Mraba wa Oktyabrskaya ulioko katikati ya mji wa Minsk ulikuwa umezungushiwa waya na vikosi vya usalama, uwanja wa uhuru pia ulifungwa kuzuia waandamanaji.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2