VISA VYA MAAMBUKIZI YA CORONA VYAONGEZEKA DUNIANI | Tarimo Blog

Na Lusajo Frank, Michuzi TV
SHIRIKA la Afya Ulimwenguni (WHO) limeripoti idadi kubwa ya visa vya virusi Corona ulimwenguni na visa 307,930 vimethibitishwa kwa siku moja.

Jimbo Victoria ni la pili lenye idadi kubwa ya watu nchini Australia na kitovu cha mlipuko wa virusi Corona nchini humo, 

Vimeripotiwa visa 35 vipya ambavy ni ongezeko la chini zaidi la kila siku katika miezi mitatu.

Zaidi ya watu milioni 28.9 kote ulimwenguni wamegundulika kuwa na virusi corona na zaidi ya 922,000 wamefariki duni, kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Karibu watu milioni 19.5 wamepona.

Janga la Corona lilikumba dunia mnamo 31 Desemba 2019, inayojulikana rasmi kama COVID-19. Virusi vilitengwa kwa mara ya kwanza na watu wenye homa ya mapafu katika mji wa Wuhan, nchini China.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2