PROF. MDOE AITAKA TEWW KUANDIKA MAANDIKO YA KIBUNIFU | Tarimo Blog


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe (katikati) akizundua mpango mkakati wa Kitaifa wa miaka mitano wa kukuza na kuendeleza kisomo na elimu kwa Umma, kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Dkt. Michael Ng'umbi na kushoto ni  Mwenyekiti wa Baraza la  Usimamizi la TEWW Dkt. Naomi Katunzi.
Mkurugenzi wa Taasisi yw Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Dkt. Michael Ng'umbi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza na Kuendeleza Kisomo na Elimu kwa Umma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe wakati wa maadhimisho ya kielele cha Juma la  Elimu ya Watu Wazima duniani na uzinduzi wa mkakati wa Kitaifa wa kukuza na kuendeleza kisomo na elimu kwa Umma nchini Tanzania.


Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe ameitaka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kuwa wabunifu zaidi kwa kuandika maandiko yatakayowaletea fedha zitakazotumika kutekeleza shughuli mbalimbali zilizopo katika mkakati wa Kitaifa wa kukuza na kuendeleza kisomo na elimu kwa Umma.

Profesa Mdoe amesema hayo leo Septemba 25/2020 kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Leonard Akwilapo wakati wa maadhimisho ya kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima duniani na uzinduzi wa mkakati wa Kitaifa wa kukuza na kuendeleza kisomo na elimu kwa Umma nchini.

Aidha, Profesa Mdoe amewahakikishia kuwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu itaunga mkono TEWW katika kuhakikisha malengo yaliyowekwa katika mkakati huo yanafikiwa kwa kiasi na ufanisi mkubwa.

"Nimeelezwa kuwa TEWW inakabiliana na changamoto ya ufinyu wa bajeti zinazokwamisha kuwafikia walengwa wengi, kwa hiyo niendelee kuwahimiza kutumia fedha za ndani kwa kutumia vyanzo vya ndani pamoja na kuwa wabunifu," amesema Profesa Mdoe

Amesema ni matumaini yake kuwa mkakati huo utapunguza idadi na viwango vya vijana na watu wazima wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu nchini kwa kuwajengea uwezo wa kuyatambua, kuyatafsiri na kuchukua hatua sahihi za kukabiliana na changamoto zilizokuwepo kwenye mazingira yao.

"Nitoe rai kwa TEWW ambapo ndiyo waratibu wakuu wa mpango huu kusimamia vema ili watekelezaji wakiwemo TAMISEMI na wadau wengine wautekeleze kama ilivyopangwa," amesema

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt. Michael Ng'umbi amesema pindi wahitimu wa programu za elimu ya watu wazima wanapomaliza masomo yao wanashiriki katika uwezeshaji wa madarasa ya kisomo na kuasaidia kwa kiasi kikubwa katika jitiada za Serikali za kupunguza tatizo la kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).

Dkt.Ng'mbi amesema kwa TEWW imeweka utaratibu wa wanachuo wanapokuwa natoka mafunzo kwa vitendo kuanzisha na kuwezesha madarasa ya kisomo sehemu mbalimbali nchini kwa kipindi chote wanapokuwa natoka mafunzo hayo.

Pia, amesema TEWW imekuwa ikishirikiana na wadau wa maendeleo katika kuendesha miradi na programu mbalimbali za elimu  ya watu wazima nchini, ambapo wadau hao ni UNICEF, UNESCO, Brac-Maendeleo, COL, Benki ya Dunia na KOICA.

"Utekelezaji wa miradi na programu hizi umewasaidia vijana na watu wazima walionufaika kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kisiasa, kijamii na kiuchumi, hivyo kuunga mkono jitiada za Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli." amesema.

Amesema mkakati huo wa Kitaifa wa miaka mitano 2020/2021 hadi 2024-2025 wa kukuza na kuendeleza kisomo na Elimu kwa Umma, ambapo mkakati huo unalenga kupunguza idadi ya vijana na watu wazima wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu wanaokadiriwa kuwa milioni 5.5 kulingana na sensa ya 2014.

Dkt.Ng'umbi amesema mkakati huo uliozinduliwa unalenga kuandaa programu za kutosha kwa watu mbalimbali, mifumo ya programu wezeshi, ukusanyaji wa takwimu, kuweka viwango vya sifa, kuandaa zana za kutosha, kuandaa wawezeshaji wa Elimu na kisomo na kuendeleza utafiti.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi la TEWW, Dkt. Naomi Katunzi amesema anamshukuru sana Katibu Mkuu, Dkt. Akwilapo kwa kuweza kushughulikia mkakati huo ndani ya wiki moja na kuweza kuzinduliwa, ambapo mkakati huo ulikwama kwa muda mrefu bila majibu.

Amesema ni lengo ni kupeleka elimu kwa wananchi, kwa kuwapelekea elimu mbadala ya watu wazima, nia na lengo mkakati huo usonge mbele, ambapo ameahidi kuufutilia makakati kwa  kuhakikisha Taasisi inakwenda mbele zaidi kwa kusambaza elimu.

Pia  Mkuu wa Kitengo cha Elimu,UNESCO Tanzania, akiwamuwakilisha Mkurugenzi Torso Dos Santos, Faith Shayo amesema kauli mbiu ya mwaka huu inalenga kufundisha, kusoma, kuhesabu na kuzingatia majukumu ya ufundishaji.

Amesema UNESCO itaendelea kuiunga mkono Taasisi hiyo ili iendelee kutoa elimu ya watu wazima sehemu mbalimbali hapa nchini na kufikia maeneo mengi kwa wakati mfupi.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2