Na Farida Saidy, Michuzi TV, Morogoro
BAADA ya watanzania kusubri kwa muda mrefu kufunguliwa kwa bucha za Wanyayapori hapa nchini hatimaye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce K.Nzuki, ametangaza rasmi maeneo ya kuanzisha bucha za Wanyamapori.
Akitoa taarifa hiyo mbele waandishi wa habari leo katika Ofisi za makao makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania( TAWA) Mkoani Morogoro, Katibu Mkuu huyo ametangaza Mikoa 23 ya Tanzania Bara ambayo itaanza kufungua Bucha za wanayapori.
Amesema kuwa Mikoa iliyosalia ikiwemo Mikoa ya Songwe, Mara na Rukwa nayo itapewa fursa ya kuuza kitoweo hicho baada ya kukamilika kwa utaratibu wa kiutendaji ambao umewekwa na mamlaka hiyo.
Sambamba na uanzishwaji wa majengo ya bucha za Wanyamapori,Wizara imeweka vigezo vya Magari maalum yatakayotumika kubeba na kuuza Nyamapori(mobile butcher) katika maeneo mbalimbali nchini.
Hata hivyo ameeleza kuwa mpaka sasa TAWA imepokea jumla ya maombi 25 ya watanzania wanaokusudia kuanzisha bucha za Wanyamapori, na amewataka watu kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa ya kutuma maombi ndani ya siku 14 kuanzia tarehe 25.09.2020 ili kuwahi kalenda ya vikao vya kamati ya kupitisha maombi,ambayo inakutana mara nne kwa mwaka.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment