RAIS JOHN MAGUFULI ASEMA MATUNDA YA UWANJA WA CHATO YAMEANZA KUONEKANA | Tarimo Blog

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Chato

RAIS Dk.John Magufuli amesema waliokuwa wakihoji kuhusu uwanja wa ndege wa Chato sasa wataanza kujifunza kwamba uwanja huo umeanza kutoa matunda.

Ametoa kauli hiyo leo Septemba 13, 2020 akiwa katika uwanja huo wa Chato ambako ndiko limefanyika tukio la kihistoria la uitiwaji saini wa waraka wa pamoja wa makubaliano ya kusudio la utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanzania.

Utiwaji saini huo umefanywa na Rais Magufuli pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Rais Museveni aliwasili Chato kwa kutumia usafiri wa ndege ambapo ilitua katika uwanja .Tukio hilo lilifanyika uwanjani hapo na kuhudhuria na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali wa nchi hizo mbili.

Hibvyo wakati Rais Magufuli akiendelea kuzungumza kuhusu bomba hilo, amesema Rais Museveni ametua kwenye uwanja huo wa Chato."Wanaopinga kuwepo kwa uwanja huo wataanza kujifunza uwanja huu umeanza kutoa matunda.Uwepo wa uwanja wa ndege huo umesaidia kufanikisha jambo hilo bila kuchelewa.

Wakati huo huo Dk.Magufuli amewaomba wanachi wa Uganda kumtunza Rais Museveni kutokana na maono yake."Maono yake yamesaidia Tanzania kupata mabilioni ya fedha.Nakutakia mafanikio mema kwa yale yote unayotaka kuyafanya"amesema.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2