Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Chato
WAKATI kampeni za Uchaguzi Mkuu zikiendelea nchini, Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemwambia Dk.John Magufuli atashinda uchaguzi huo na kwamba atamuombea kwa Mungu ili ashinde.
Akizungumza jana wilayani Chato mkoani Geita baada ya tukio la utiaji saini wa Waraka wa Pamoja wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, Rais Museveni amesema anafahamu kuwa Dk.Magufuli na Chama chake cha CCM wako katika kampeni za kuomba kura.
“Najua Rais Magufuli anatafuta kura, nitamuombea kwa Mungu na atashinda."amesema Rais Museveni huku mamia ya wana CCM waliokuwepo kwenye tukio hilo wakishangilia.
Mbali ya kumuombea Dk.Magufuli na Chama chake washinde katika uchaguzi huo, Rais Museveni amesema kila anapokuja Tanzania amekuwa akimbuka mambo ya zamani na ya sasa.
"Wakati nakuja nilikuwa nasikiliza nyimbo za zamani nadhana za enzi za TANU, kwa hiyo nitafurahi kama nitapewa hizo nyimbo kwenye flashi,"amesema.Nyimbo hizo ni Tazama ramani na Tanzania Tanzania.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment