YANGA YATAKATA KWA MKAPA NA UZI MPYA | Tarimo Blog

Yassir Simba, Michuzi TV

Uzi mpya wa Yanga waja na baraka zake kwa Mkapa huku Yanga wakimchakaza Mbeya City kwa bao 1-0.

Ligi kuu Tanzania bara VPL imeendelea tena leo Septemba 13,2020 huku Yanga wakitaka na uzi mpya Yani jezi mpya kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wanakoma kumwanya Mbeya City, bao la dakika ya 86 likifungwa na beki kisiki wa Yanga Lamine Moro akiunganisha mpira wa Kona uliopigwa na Carlinhos na kuipatia Yanga bao la kuongoza na la ushindi katika mchezo huo.

Mchezo huo uliotawaliwa na ufundi na mbinu kwa asilimia kubwa huku Yanga wakiingia katika mchezo huo na mabadiliko katika kikosi chao wakianza na Lamine Moro,Haruna Niyonzima,Mukoko Tonombe pamoja na Tuisila Kisinda ambao walikuwa chachu ya mabadiliko katika kikosi hicho huku Saprong pamoja Yacouba  wakifanya majaribio kadhaa ambayo mlinda mlango wa Mbeya City Haroun Mandanda akifanya kazi kubwa kuzuia mashambulizi ya Yanga.

Mabadiliko yaliyofanywa na Yanga kumtoa Feisal Salum na nafasi yake kuchukuliwa na Carlinhos ambaye alifanya kazi kubwa katika mchezo huo huku akitoa pasi ya goli ambalo limewapa Yanga alama tatu muhimu katika mchezo huo.

Baada ya ushindi huo Yanga wanashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 4 magoli 2 katika michezo miwili waliocheza huku Mbeya City wao wakiburuza mkia katika nafasi ya mwisho nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi.








 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2