RAIS MUSEVENI ATAJA HATUA KWA HATUA WALIVYOFANIKISHA KUYAPATA MAFUTA... | Tarimo Blog

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Chato
RAIS wa Uganda Yoweri Museveni ameeleza hatua kwa hatua kuhusu juhudi walizofanya kuhakikisha wanapata mafuta ambayo sasa baada ya kukamilika kwa bomba la kuyasafirisha kutoka nchi kwake hadi Tanzania yataanza kwenda kuuzwa kwenye soko la Dunia.
Ameyasema hayo leo Septemba 13,2020 wilayani Chato mkoani Geita wakati akizungumzia ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania.
Ambapo ametumia nafasi hiyo kusisitiza kwamba takwimu ambazo zimetolewa na Rais Dk.John Magufuli kuhusu yale ambayo wamekubaliana ziko sawa.
"Sasa juu ya bomba, Rais Magufuli amelizungumzia vizuri na takwimu zote wamezionesha, mapipa ya mafuta  bilioni 6.5 ambayo ndio mafuta yanajulikana kwa sasa na eneo ambalo limegundulika kuwa na mafuta ni asilimia 40 kati ya eneo lote na ambalo limebakia tunaendelea kutafuta na matarajio yao ni kupata mafuta mengi zaidi.
"Pia kuna sehemu nyingine imebainika kuwa na mafuta.Bonde Albarti tunayo mafuta tayari kwani yanayonekana kwenye kompyuta, lakini shida iliyoko kuna fujo kule , hatujapata muda wa kufuatilia.
"Wakati tunatafuta mafuta tulishirikiana na Mabutu alipokuwa madarakani lakini ikashindana na baadae tukaona tufanye peke yetu.Tumetumia watalaamu wetu mwanzo mpaka mwisho, watu wa nje walituchezea,"amesema Rais Museveni wakati anafafanua jinsi walivyogundua mafuta.
Ameongeza kuwa Ulaya Mashariki baada ya kuanguka, nchi ya Urusi nayo ilibaini inayo mafuta mengi sana ,hivyo kampuni nyingi za kutafiti mafuta zikaelekeza nguvu katika nchi hiyo na wakaisahau Uganda.
"Wakawa wanasema wana wasiwasi mafuta hayapo.Wakabadilika na kutuambia mafuta hayapo, tukahoji sasa mbona wametugeuka, tukaamua kuagana nao.Hivyo tukapeleka watu wetu kwenda kusoma nje na baada ya kurudi ndio wakafanya kazi hiyo na leo tunamafuta,"amesema.
Amesema mafuta yaligundulika mwaka 2006, hivyo sasa ingekuwa imefika miaka 16 wanaendelea kuvutana na kampuni za mafuta na ingawa wamechelewa lakini wamejifunza zaidi juu ya mafuta.
Kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, Rais Museveni amesema watu wake walikuwa wanagombania kodi ambazo ndani ya miaka 25 zinakuwa dola milioni 800, lakini huo mradi uwekezaji peke yake ni dola bilioni 16 kwa pande zote mbili,
"Hivyo nimeona hakuna sababu ya kuendelea kuchelewesha mradi huu kwasababu ya kodi.Ni kama vile unapoanza shamba jipya na ukaanza kulima kwa mara ya kwanza litakuwa na gharama lakini utakapolima tea gharama zitapungua.
"Tuanze kupata hasara ya hapa na pale, tukashaingia tutajifunza zaidi, tutapa fedha za kuendesha mambo mengine.Hawa watu wangu ni wakali kwa Wazungu, niliwafundisha ukali na hiyo ni safi sana,"amesema Rais Museveni.
Akifafanua zaidi Rais Museveni amesema alizungumza na Rais Magufuli kwa simu kuhusu namna gani watagawana juu ya mrad."Kwasababu kama ambavyo mmesikia sehemu kubwa mradi uko Tanzania.
"Kwa hiyo nielezea kama unataka kuchukua asilimia 70 kwa asilimia 100 we chukua tu, kama ni asilimia 80 kwa asilimia 100 ni nyingi sana. Tumekubaliana 60 inakuja Tanzania na 40 inakwenda Uganda, kwa hiyo nafurahi.Kama mnavyosikia hivi karibuni tutakuja kuzungumzia gesi, Uganda tunamahitaji ya gesi.
"Uganda inaonekana kuwa na mafuta, gesi ipo lakini ni kidogo, tunataka gasi kwa ajili ya vyuma vya pua na mambo mengine, kwa hiyo nashukuru ile ofa yako Rais Magufuli kwamba pale bomba la mafuta litapita basi bomba la gesi litapita, sasa huo ndio undugu,amesema Rais Museveni.
 Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiongea baada ya kutia saini Waraka wa Pamoja Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2