*Mgombea Udiwani kata ya Mbezi Ismail Malata aahidi makubwa kwa Wanambezi
Chama cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Ubungo Kimesema kazi yake wamajipanga kurudisha kata zote na majimbo yaliyokuwa yametwaliwa na vyama vya upinzani.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja wakati akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Mbezi Ismail Malata jijini Dar es Salaam.
Mgonja amesema kuwa ilani ya chama cha Mapinduzi kimeweka wazi katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kukuza uchumi wa mtu mmoja kwa wananchi wa kata ya Mbezi pamoja na Wilaya nzima kwa ujumla .
Amesema kuwa wananchi wa mbezi wanachangamoto ya barabara hivyo Diwani Ismail Malata ndio atapigana katika kuleta barabara hiyo kwa kuwasilisha katika baraza la madiwani.
Amesema Kata hiyo na majimbo yalikuwa na wapinzani na hakuna maendeleo hivyo wananchi wapige kura kwa kuchagua mafiga matatu yaani Rais wa CCM,Mbunge wa CCM pamoja na Diwani wa CCM.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Mbezi Ismail Malata amesema kuwa amekuwa na uchungu sana kuona maendeleo hayapatikani Kata ya Mbezi ni kutokana na wapinzani kurudisha nyuma maendeleo hayo.
Amesema akichaguliwa atakuwa kiungo kikubwa katika kutatua maendeleo ikiwemo Barabara, Afya,Maji vinapatikana.
Amesema mipango yake iko mengi lakini kura za wananchi Oktoba 28 zitaamua kufanya maendeleo hayo yapatikane.
Malata amesema kata hiyo ilikuwa 'Nchi ya Misri' yaani hakuna kilichofanyika bali aliyekuwepo aliangalia masilahi yake na kuwaacha wananchi waliomchagua.
Aidha amesema kura zote za wanambezi wampe ili kuweza kupata maendeleo kutokana na ilani ya chama cha Mapinduzi ilivyojipambanua katika kutumikia wananchi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akizungumza na wananchi kuhusiana na ilani ya chama cha mapinduzi kilivyojipanga katika kuwatumikia wananchi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akizungumza na wananchi kuhusiana na ilani ya chama cha mapinduzi kilivyojipanga katika kuwatumikia wananchi.
Mgombea Udiwani Kata ya Mbezi Ismail Malata akizungumza na wananchi wakati wa kuomba kura kwa wanambezi katika uzinduzi wa kampeni wa kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wanachama wa CCM wakisikiliza sera
Picha mbalimbali katika uzinduzi wa Kampeni za mgombea Udiwani kata ya Mbezi
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment