MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi maalum muhitimu Abdulrahman Abdalla aliyefaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza masomo ya biashara kutoka Skuli ya Sekondari ya Biashara Mombasa Zanzibar.
BAADHI ya Wahitimu wa kidato cha sita waliofaulu mitihani yao kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika Verde.
***********************************
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesesema uchumi imara wa nchi unatokana na uwepo wa wasomi wa fani mbalimbali wenye uwezo wa kupanga mikakati madhubuti ya kimaendeleo.
Kauli hiyo ameitoa leo katika hafla ya kuwapongeza Wahitimu wa kidato cha Sita waliofaulu mitihani yao kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu mwaka 2020 Zanzibar,iliyoandaliwa na Afisi Kuu ya CCM Zanzibar ambayo imefanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Unguja.
Dk.Mwinyi, amesema elimu ndio msingi wa maendeleo ya binadamu yeyote hivyo ni lazima wahitimu hao waendelee kusoma kwa bidii ili wafike ngazi ya elimu ya juu kitaaluma.
Kupitia hafla hiyo Dk.Mwinyi, ameeleza kwamba endapo atapewa ridhaa na wananchi kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi atalipa kipaumbele suala la kuimarisha sekta ya elimu nchini.
Alisema akipata nafasi hiyo ataupitia upya mfumo wa elimu nchini ili uende sambamba na dhamira ya uchumi mpya wa Zanzibar.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa amepanga kutekeleza mambo matano katika sekta hiyo yatakayomaliza changamoto katika sekta hiyo.
Amesema jambo la mwanzo ni kutazama upya miundombinu ya elimu yakiwemo majengo kuanzia ngazi za msingi hadi vyuo vikuu kwani wanafunzi wanatakiwa kusoma katika majengo bora na ya kisasa.
Pia amesema jambo jingine ni uwepo wa Rasilimali watu ya kutoka wakiwemo walimu wenye sifa na idadi yao inaendana na mahitaji ya kielimu sambamba na kusimamia maslahi yao.
Dk.Mwinyi, amesema ni kuhakikisha anaweka mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia vikiwemo vitabu na vifaa mbalimbali vinavyomuwezesha mwanafunzi kusoma kwa uhuru akiwa na mahitaji yote ya msingi.
Sambamba na hayo alisema lazima elimu igharamiwe kwa kutizama upya bajeti ya elimu ili iendane na mahitaji ya walimu hao.
Mgombea huyo, alilitaja jambo la tano kuwa ni lazima kufanyike takwimu za kitaalamu zitakazofanyia utafiti wa kina kubaini idadi gani ya walimu wanahitajika sambamba na mahitaji mengine ya vifaa.
Amesema mambo hayo yakifanyiwa kazi itapatikana elimu bora na kwamba serikali itaendelea kuwataka vijana wengi wa kujiunga na vyuo vya ufundi.
Ameeleza kuwa serikali itaweka mkazo katika udahili na kuongeza udhamini kwa wanafunzi pamoja idadi ya walimu wanaohitajika katika ngazi za Vyuo vikuu.
Aidha, amewasihi wananchi kutunza amani na utulivu wa nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo octoba 28 mwaka huu ili kutekeleza haki yao ya kidemokrasia.
”Maendeleo ya Zanzibar yanategemea sana uwepo wa amani na utulivu hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kulinda Amani hii tuliyokuwa nayo isituponyoke”, alisema Dk.Mwinyi.
Naye Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Tabia Maulid Mwita, amesema vijana ndio jeshi la ushindi la Chama cha Mapinduzi hivyo watahakikisha CCM inashinda kwa kishindo.
Amesema bado vijana wengi wanahitaji fursa ya za elimu ili wapate taaluma mbali mbali zitakazowasaidia katika maisha yao ya sasa na baadae.
Pamoja na hayo alimpongeza Mgombea huyo kwa hotuba yake aliyotoa jana katika uzinduzi wa kampeni za CCM Zanzibar na kueleza kuwa ilijaa maono ya kuendelea kuijenga Zanzibar kiuchumi.
Kwa upande wake,Mratibu wa Elimu,Ajira na Mafunzo kutoka Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Khamis Abdi, amesema Afisi Kuu ya CCM Zanzibar imejipangia utaratibu Maalum wa kila mwaka kuwapongeza wahitimu waliofanya vizuri katika mitihani yao.
Ameeleza kuwa utaratibu huo wa kuwapongeza wanafunzi wanaofaulu kwa kiwango cha daraja la I-III toka mwaka 2017 kwa lengo la kuwatia moyo vijana hao ili waendelee kusoma kwa bidii.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud, akitoa mada ya msomi wa kimapinduzi na maendeleo ya Taifa,amesema wahitimu hao ndio watapatikana viongozi,watendaji na wataalamu wa fani mbali mbali katika ijay
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment