Taasisi yaanza kuhamasisha utalii wa ndani kutumia wanafunzi | Tarimo Blog

Taasisi ya Chem chem association ambayo imewekeza shughuli za kitalii, katika eneo la la Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori(WMA) ya Burunge,wilaya ya Babati mkoa wa Manyara, imeanzisha mpango wa kuhamasisha utalii wa ndani, kwa kupeleka wanafunzi kujionea vivutio vya utalii ili baadaye waje kuwa mabalozi wa utalii na kupiga vita ujangili.


Hatua hiyo, imechukuliwa kuunga jitihada za serikali kukuza utalii wa ndani hasa baada ya watalii kupungua kutokana na athari za Corona  duniani na tayari wizara ya maliasili na Utalii, kupitia katibu Mkuu wake, Dk Aloyce Nzuki ameshauri taasisi za uhifadhi kuhamasisha utalii wa ndani.


Akizungumza na kundi la wanafunzi wa kituo cha kulea  watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mdori wilayani Babatia, Mwongoza watalii wa taasisi ya chem chem,  Salum Mpampa alisema wameamua kuanza kuhamasisha wanafunzi kupenda utalii na uhifadhi ili waje kuwa mabalozi katika sekta hiyo.


"kundi hili la wanafunzi kutoka kituo cha  TGCWC ni mfululizo ya makundi ya wanafunzi ambao tumeanza kuwaleta kutembea hifadhi hii ili kujionea faida za utalii lakini pia kutambua rasilimali ambayo mungu amelijalia taifa hili kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo"alisema


Alisema wanafunzi hao, wanapata fursa kuona wanyama mbali mbali, kupata elimu ya uhifadhi lakini pia wanapata fursa ya kuuliza maswali kuhusiana na masuala ya uhifadhi.


Mlezi wa kituo hicho, Sipora Paulo alisema wamejifunza mambo mengi katika hifadhi hiyo, ambayo ipo kati kati mwa hifadhi ya Tarangire na Manyara.


"tumeona wanyama wengi sana, tumejifunza maisha yao lakini tumeona faida ya uwekezaji wa taasisi ya chemchem katika hifadhi hii"alisema


Mmoja wa wanafunzi hao, Rahma Ally alieleza kushukuru kuwa mmoja wa wanafunzi waliotembelea hifadhi hiyo na kujionea vivutio vya utalii na akashauri wanafunzi wengi zaidi kujitokeza kutembea.


 Wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa wanatembeleahifadhi ya jamii ya Burunge kujionea vivutio vya utalii.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2