Watu wanalalamika bila ya kuwa na idhibati.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa halina mgongano wa kimaslahi ambao unatokea pale wanapotekeleza majukumu yao.
Shirika hilo limesema hayo kutokana na watu wanatengeneza taarifa juu utoaji huduma kuwa na mapungufu ,wakati uwepo wa shirika ni kwa mujibu wa sheria na utendaji wake hauingiliani na taasisi zingine katika utoaji huduma na hawashindani ma mtu yeyote.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Emmanuel Ndomba amesema shirika hilo limekuwa likikejeliwa kutotekeleza kazi zake kiuweledi huku wengi wakienda mbali zaidi wakilishutumiu shirika hilo kuwa halina watendaji wenye uweledi.
Ndomba amesema kuwa watu wanalalamika lakini hawana idhibati ya kile wanacholalamika nacho na Taasisi ikilalamikiwa ni kunahitaji kutoa ufafanuzi.
“Kuna nia ovu inayoenezwa kuwa TASAC haina wataalamu wenye ujuzi wakati wataalamu wenye uweledi 306 walioajiriwa na wengine zaidi ya 120 wa muda mfupi na tayari tumesajili meli 375 katika kipindi kifupi cha utendaji wetu huu ni mwaka mmoja tu tangu tuanze kazi haya ni maendeleo makubwa”alisema.
Ndomba amesema mbali na uvumi huo kumekuwa na taarifa kuwa TASAC haiingii mikataba na wnye meli hivyo utendaji wake si wenye kuzingatia uweledi.
“Meli zinapokuja ambazo haziko katika safari za mara kwa mara hapa nchini maana yake tumeshapokea barua pepe kutoka kampuni husika hivyo hakuna haja ya kuingia mikataba tena hiyo ni mifumo ya zamani lazima tufanye kazi kulingana na mabadiliko ya teknolojia”alisema.
Ndomba amesema watu wanaovumisha taarifa hizo wanalengo la kuichafua TASAC huku akisisitiza kuwa hakuna muingiliano wa majukumu yeyote wa kiunedeji baina ya shirika hilo na taasisi binafsi.
Pia wanavumisha kwamba gharama tunazotoza kwa kontena linaloingia baharini ni kubwa,wameenda mbali zaidi kutusukuma kuanza kutoza ambapo meli zitatozwa sh 2 wakati huduma hiyo awali ilikuwa wanatozwa kutoka Dola nane hadi 14.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC) Emmanuel Ndomba akizungumza na waandishi habari kuhusiana na malalamiko dhidi yao katika utoaji huduma ,jijini Dar es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment