DPP- AMANI NA USALAMA WA TAIFA NI JUKUMU LA KILA RAIA | Tarimo Blog

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MKURUGENZI wa mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amesema Amani na Usalama wa Taifa la nchi ya Tanzania ni jukumu la kila raia, mtanzania ama raia wa kigeni aliyeko nchini.

Amesema, siyo tu jukumu la vyombo pekee vilivyopewa mamlaka ya kuweza kutunza..., siyo vile vya Ulinzi na Amani, Mahakama au Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ni jukumu la kila mmoja wetu kwa sababu amani na usalama vikitoweka kila mmoja kwa njia moja ama nyingine ataathirika na pia huwezi kuwa na nchi yenye Maendeleo bila ya kuwa na Haki, Amani na Usalama 

DPP Mganga ameyasema hayo leo Septemba 17 wakati wa kikao chake na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari kilichofanyika katika ofisi yake jijini Dar es Salaam, 

Amesema lengo kubwa la kuwapo kwa ofisi ya ya mashtaka katika nchi zote duniani ni kusaidiana na vyombo vyote vinavyoshughulika na upelelezi ili kuhakikisha kwamba nchi inakuwa na amani na utulivu.

"Lengo kubwa la kuwepo kwa ofisi ya mashtaka ni kuhakikisha watu hawavunji sheria, watu wanafuata sheria na nchi inakuwa na amani na usalama ambapo ukiyachukua yote hayo kwa pamoja utakuta lengo Kuu ni kuwa na utawala wa sheria ili kusiwepo na nchi ambayo kila mmoja anajichukulia sheria kwa jinsi anavyotaka." Amesema DPP

Amesema kumekuwepo na misemo kutoka kwa watu wengi wakiwa wanasema wanaenda kwenye ofisi ya DPP, lakini kwa uelewa wake ukisema ofisi ya DPP ni chumba anachotumia yeye kama ofisi lakini ofisi iliyopo ni ofisi ya Taifa ya mashtaka ambayo majukumu yake ni kuendesha mashtaka ama kesi za jinai hapa nchini ambayo pia ina majukumu yake Kikatiba.

Pia Mganga amesema, toka kuanzishwa kwa ofisi hiyo wamefanikiwa kudhibiti wizi wa mtandao na pia wameweza kudhibiti vitendo vya ukatili wa mauaji kwa Albino ambapo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ni kesi tano tu zilizofunguliwa ambapo kesi nne zimekwishamalizwa kwa watuhumiwa kutiwa hatiani na nyingine moja iko kwenye hatua ya usikilizwaji

Aidha amewaasa wazazi wanaoshirikiana na wanaume wenye tabia za ubakaji na kuwaoza binti zao au kuharibu ushahidi wa watoto wao kubakwa, kuacha mara moja kwani wakikamatwa watachukuliwa hatua kali ikiweno kuwekwa ndani wazazi wa aina hiyo.

DPP amewataka pia wananchi wanaokumbana na kero mbalimbali zinazoigusa ofisi yake, ikiwamo kuchelewa kwa upelelezi ama watuhumiwa kuwekwa mahabusu kwenye vituo vya polisi, kufika kwenye ofisi zao na kutoa malalamiko yao ambayo ameahidi yatashughulikiwa haraka.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa utaifishaji wa mali makosa yanayovuka mipaka na uhalifu mahsusi, Paul Kadushi amedai, mbali na changamoto mbali mbali, sekta hiyo pia imekuwa na mafanikio mbali mbali ambapo nchi imeweza kupata amri ya utaifishaji mali zilizotokana na makosa mbali mbali ikiwemo ujangili, dawa za kulevya na utoroshaji wa madini.

"Mpaka sasa Magari 143, pikipiki 163, nyumba 23 na viwanja 10 kutoka maeneo tofauti ya nchi, yametaifishwa huku Kwenye madini, tani 84.07 zenye thamani ya Sh. bilioni 45.82. Ambazo kati yake madini ya vito ni tani 83.596 yenye thamani ya Sh. bilioni sita na Kg 425 za dhahabu zenye thamani ya Sh. bilioni 38.9. Pia tumetaifisha magogo 18,409 yenye thamani ya Sh. bilioni 1.15, amesema Kadushi

Naye Mkurugenzi wa Divisheni ya Usimamizi wa Kesi na Uratibu wa Upelelezi, Hashim Ngole, ameyataja mafanikio mengine ya ofisi hiyo ni kuharakisha upelelezi wa kesi na 

Kuongeza kuwa katika kuhakikisha wanapunguza msongamano wa mahabusu kwenye magereza mbalimbali nchini, waliwezesha kufanyika kwa marekebisho ya sheria ili kuweka kifungu kinachoruhusu watuhumiwa kukutana na DPP na kuomba kukiri makosa.
Mkurugenzi w utaifishaji mali, makosa yanayovuka impala na uhalifu mahsusi, Paul Kadushi akizungumza katika kikao cha DPP na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar ves Salaam.
Mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania, Biswalo Mganga akifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwa wahariri wa vyombovya habari na wakurugenzi wa divisheni tofauti katika ofisi ya Taifa ya Mashataka. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa divisheni ya kusimamia utenganishaji wa shughuli za mashtaka, Oswald Tibabyekomya.
Mkurugenzi wa divisheni ya usimamizi wa kesi na uratibu wa upelelezi , Hashim Ngole akiwasilisha mada katika kikao hicho. Kushoto ni  Mkurugenzi wa divisheni ya makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha na rushwa Rosemary Shio.
baadhi ya wahariri wa habari wakifuatilia kikao hicho.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2