TUME KUTOA RUFAA NA MALALAMIKO YA WATUMISHI WA UMMA | Tarimo Blog



TUME ya Utumishi wa Umma inataraji kutoa baadhi ya rufaa na malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na watumishi wa Umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na waajiri na mamlaka zao za nidhamu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imeelezwa kuwa rufaa na malalamiko hayo yaliyotolewa na waajiri na Mamlaka zao za nidhamu yatatolewa uamuzi na Tume kwenye mkutano namba 1 wa mwaka wa fedha 2020/2021 ulioanza leo Septemba 21 na kuhitimishwa Oktoba 2020 jijini Dar es Salaam.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa shughuli nyingine zitakazofanyika katika mkutano huo ni pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa kipindi cha robo tatu (Januari hadi Machi) na robo ya nne (Aprili hadi Juni) ya mwaka wa fedha 2019/2020.

Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa Tume inatekeleza majukumu hayo kwa mujibu wa kifungu cha 10 (1) cha sheria ya utumishi wa Umma sura ya 298.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2