Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wenye Viwanda na Biashara Tanzania (TWCC) Jacquiline Maleko akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa tuzo za wanawake kwenye sekta ya viwanda na Biashara jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza (mwenye kipaza sauti) akizungumza kuhusiana na utaratibu wa ushiriki wanawake katika tuzo ,jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
CHAMA Cha Wanawake Wenye Viwanda na Biashara Tanzania (TWCC) kimezindua Tuzo za Wanawake waliofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2020 katika sekta za Viwanda na Biashara.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho Jacquiline Maleko amesema kuwa Tuzo hizo ni za kutambua na kuheshimu wanawake waliofanikiwa na wale wanaochipukia katika sekta ya viwanda na biashara.
Amesema katika tuzohizo licha ya kuwatambua pia ni kujenga imani juu ya ujasiriamali na kuhamasisha wanawake wa vizazi vijavyo kuwekeza na kujishughulisha katika shughuli za wawanda na biashara pamoja na kusherekea mafanikio waliyopata wanawake katika sekta hizo.
Maleko amesema Tuzo hizo zinalenga kuonesha mchango wa mwanamke mjasiriamali katika kukuza uchumi wa nchi na kuchochea maendeleo ya Jamii na kuongeza kuwa wanawake ni nguzo muhimu sana katika maendeleo ya jamii yeyote na kwamba wanawake wa uwezo wa kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda na biashara endapo wataaminiwa na kupewa nafasi ya kufanya hivyo.
Maleko amesema serikali imeweka mazingira wezeshi kwa kuendelea kuboresha biashara nchini ambapo wanawake wameweza kuanzisha biashara na viwanda vodogo vidogo ambavyo vimeongeza vipato, kuzalisha ajira pamoja na kuchangia katika ukuaji wa uchumi.
Amesema fomu za tuzo hizo zitapatikana katika tovuti ya https://bit.ly/35msDki za serikali Mikoa ,Wilaya ,Ofisi za TWCC za Mikoa na Makao Makuu na zoezi hilo litafungwa Oktoba 9 mwaka huu na utoaji wa tuzo za washindi na sherehe linatarajiwa kufanyika Novemba 28 mwaka huu.
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza amesema Tuzo hizo zimefadhiliwa na TradeMark East Africa chini ya mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wa kufanya biashara .
Amesema kuwa mradi huo unagharimu Bilioni mbili kwa miaka mitano ambapo umeanza mwaka 2018 na umewafikia wanawake 3000 na lengo ni kuwafikia wanawake 10000 kuwafanikisha kuwajengea uwezo wanawake wa Tanzania kufanya biashara.
Amesema kuwa wanawake wanaweza kujiunga katika chama hicho kwa binafsi au kwa kutumia kampuni kwa gharama za kawaida.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment